Paulo Miki
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Paulo Miki (takriban 1565 – 5 Februari, 1597) alikuwa mtawa wa Kanisa Katoliki nchini Japani.
Ametambuliwa kuwa mtakatifu kama mfiadini.
Sikukuu yake ni tarehe 6 Februari.
[hariri] Maisha
Paulo Miki alizaliwa nchini Japani kati ya 1564 na 1566.
Alijiunga na Shirika la Yesu (Wajesuiti), akahubiri Injili kwa ufanisi.
Lakini yalipoanza madhulumu kwa Wakatoliki, yeye na wenzake 25 walikamatwa na kuteswa vikali, na hatimaye wakasulubiwa huko Nagasaki tarehe 5 Februari mwaka 1597.
[hariri] Tazama pia
[hariri] Marejeo
- "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1282
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Paulo Miki kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |