Pasha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pasha
Pasha kitunga
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Ploceidae (Ndege walio na mnasaba na kwera)
Jenasi: Malimbus
Vieillot, 1805
Ngazi za chini

Spishi 10:

Pasha ni ndege wadogo wa jenasi Malimbus katika familia Ploceidae ambao wanatokea Afrika tu. Ndege hawa wana mwenendo kama kwera. Rangi zao ni nyeusi na nyekundu au nyeusi na njano. Hula wadudu hasa. Spishi hizi hulifuma tago lao kwa majani ya manyasi na hulining'inizia kitawi. Matago yao hayapatikani katika makundi makubwa kama yale ya kwera. Jike huyataga mayai 2-4.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]