Papa Alexander VI

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Papa Alexander VI

Papa Alexander VI (1 Januari 143118 Agosti 1503) alikuwa papa kuanzia 11 Agosti 1492 hadi kifo chake. Alimfuata Papa Innocent VIII akafuatwa na Papa Pius III.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Roderic Borgia. Alikuwa papa wa pili kutoka familia ya Borgia. Callixtus III aliyekuwa Borgia wa kwanza alimsaidia mpwa wake Roderic kupanda ngazi ndani ya kanisa. Kijana asiyekuwa na mafunzo wowote wa kiroho asiyepokea ubarikio wa upadre bado alipewa cheo na mapato ya askofu mara kadhaa katika dayosisi mbalimbali. 1456 alipewa cheo cha kardinali na 1458 akapadrishwa.

Alizaa watoto na mke wake wa kando Vannozza dei Cattani akaendelea kuwaangalia na kuwatunza hata alipokuwa papa. Arusi ya binti yake Lucrecia Borgia ilisheherekewa rasmi katika jumba la kipapa la Vatikano.

Lakini kabla hajachaguliwa kuwa papa alimwacha Vannozza akaanza uhusiano na binti Giulia Farnese aliyezaa binti naye mwaka 1492 alipokuwa papa.

Mwanawe Caesare alipewa cheo cha askofu alipokuwa na umri wa miaka 16 na kardinali alipofikia miaka 18. Baadaye aliacha maisha ya kanisa akafanywa na babaye jemadari wa jeshi la papa.

Alexander VI amejulikana pia kwa azimio lake la kugawa dunia kati ya Hispania na Ureno katika mkataba wa Tordesillas mwaka 1494. Mkataba huu ulikuwa msingi wa koloni ya Kireno cha Brazil na utawala wa Hispania juu ya nchi nyengine za Amerika Kusini.

Wapinzani walimwona kama mfano mbaya wa uharibifu wa Upapa wakati wake.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Papa Alexander VI katika Kamusi Elezo ya Kikatoliki