Out of Time (Heroes)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Out of Time"
Sehemu ya Heroes

White Beard's camp explodes.
Sehemu ya. Msimu 2
Sehemu 7
Imetungwa na Aron Eli Coleite
Imeongozwa na Daniel Attias
Tayarisho la 207
Tarehe halisi ya kurushwa November 5, 2007
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
"The Line" "Four Months Ago..."
Orodha ya sehemu za Heroes

"Out of Time" ni sehemu ya saba ya msimu wa pili wa tamthilia ya ubunifu wa kisayansi inayorushwa hewani na TV ya NBC - Heroes. Ilianza kurushwa hewani kwa mara ya kwanza mnamo tar. 5 November 5, 2007.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Wakati kipengele hiki kinaanza, Takezo Kensei anamfunga Hiro katika ubao, huku sura ikitazama katika moshi ya afyuni, unamzuia Hiro asiweze kutumia vipawa vyake. Whitebeard amempa ofa Kensei kwa chochotea anachotaka ili amkamate Hiro na aongoze jeshi lake vilevile. Amechagua kutawala nusu ya Japan na kumchukua Yaeko akiwa kama binti wake mfalme. Muda mfupi baadaye, wakati walinzi wao wamevurugwa, Yaeko akajiachia huru na kutoa ile afyuni kwa Hiro.

Wakati walinzi wamerudi, Hiro anatumia nguvu yake mpya aliyoipata na kuongeza kulipua ile afyuni kwa haraka zaidi, anayeyuka kutoka eneo lile akiwa na Yaeko, na baba wa Yaeko akimweka katika sehemu ya usalama. Baadaye usiku, amejipenyeza katika jeshi la White Beard kwa lengo la kutaka kulipua silaha zake zote, huku akijikuta Kensei anamsubiria kwa hamu. Ijapokuwa Hiro bado alikuwa na imani nae, Kensei anamvamia Hiro, anamtolea upanga ili apigane. Katika mapigano, taa ikaanguka chini na moto ukaanza kupamba hadi katika eneo lenye milipuko.

Wanagundua wapo katika hatari ya kufa, Hiro anampa mkono wake Kensei ili watoroke, kitendo ambacho Kensei alikataa. Amebaki kuwa hana jinsi, Hiro anajiondokea zake kabla mambo hayajawa mabaya katika hema lile kisha anaokota kofia ya Kensei ikiwa imeharibiwa vibaya na mlipuko wa moto. Alivyokutana na Yaeko, anaonya kwamba katika jaribio la mwisho la Kensei, ilimbidi akate moyo wake kwa ajili ya kuokoa maisha ya kipenzi cha na Japani yote. Hiro anatambua ya kwamba ina mlazimu kurudi katika muda wake, na kwa mabusu ya mwisho mwisho, kenda zake!.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]