Orodha ya vitabu vya Biblia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Biblia ikiwa imefunguliwa.


Vitabu vya Biblia ya Kikristo vilivyoorodheshwa hapa chini ni vile 66 tu vinavyotambuliwa na Wakristo wote. Zingatia lakini kwamba walio wengi, hasa Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki, katika Biblia[1] wanavyoitumia wana vitabu vingine 7 vinavyoitwa Deuterokanoni, navyo vyote vimo katika Agano la Kale[2]: Yoshua Bin Sira, Kitabu cha Hekima, Kitabu cha kwanza cha Wamakabayo, Kitabu cha pili cha Wamakabayo, Tobiti, Yudithi, Baruku.

Majina ya vitabu yameandikwa hapa kufuatana na tafsiri ya Kiswahili cha kisasa maarufu kama Habari Njema. Kama kuna jina lingine limeongezeka katika mabano.

Mungu aliandika Biblia kwa mikono ya wanadamu wengi. Wanadamu hao hawakuishi pamoja ili washirikiane kazi ya kuandika. Bali waliishi katika nchi mbalimbali na kwa nyakati mbalimbali wasijuane. Waliongea lugha mbalimbali. Walitofautiana hata katika kazi zao (wengine walikuwa wachungaji wa wanyama, au wafalme, au manabii, au wavuvi wa samaki, au watoza ushuru, n.k.). Hawakujua kwamba vitabu vyao vitawekwa pamoja visomwe kama kitabu kimoja. Wengi wao hawakuelewa hata maana ya maneno waliokuwa wakiyaandika (1 Petro 1:10-12). Mungu aliwatumia wanadamu katika kuiandika Biblia akiwaongoza na Roho Mtakatifu (2 Petro 1:20-21; Matendo 4:24-25 n.k.).

Vitabu hivi havikuandikwa kwa orodha kama vilivyo katika Biblia bali viliwekwa pamoja kwa mpangilio tu.


Agano la Kale[hariri | hariri chanzo]

Vitabu vya kihistoria[hariri | hariri chanzo]

Mwanzo (Kitabu cha Kwanza cha Musa) (Mwa)
Kutoka (Kitabu cha Pili cha Musa) (Kut)
Walawi (Kitabu cha Tatu cha Musa) (Law)
Hesabu (Kitabu cha Nne cha Musa) (Hes)
Kumbukumbu la Sheria (Kumbukumbu la Torati; Kitabu cha Tano cha Musa) (Kum)
Yoshua (Yos)
Waamuzi (Amu)
Ruthu (Kitabu cha Ruthi) (Rut)
Samueli I (1 Sam)
Samueli II (2 Sam)
Wafalme I (1 Fal)
Wafalme II (2 Fal)
Mambo ya Nyakati I (1 Nya)
Mambo ya Nyakati II (2 Nya)
Ezra (Ezr)
Nehemia (Kitabu cha Pili cha Ezra) (Neh)
Esta (Est)

Vitabu vya hekima[hariri | hariri chanzo]

Yobu (Kitabu cha Ayubu) (Ayu)
Zaburi (Zab)
Methali (Met)
Mhubiri (Mhu)
Wimbo Ulio Bora (Wim)
Maombolezo (Maombolezo ya Yeremia) (Omb)

Vitabu vya kinabii[hariri | hariri chanzo]

Isaya (Isa)
Yeremia (Yer)
Ezekieli (Eze)
Danieli (Dan)
Hosea (Hos)
Yoeli (Yoe)
Amosi (Amo)
Obadia (Oba)
Yona (Yon)
Mika (Mik)
Nahumu (Nah)
Habakuki (Hab)
Sefania (Sef)
Hagai (Hag)
Zekaria (Zek)
Malaki (Mal)


Agano Jipya[3][hariri | hariri chanzo]

Vitabu vya kihistoria [4][hariri | hariri chanzo]

Injili ya Mathayo (Mt)
Injili ya Marko (Mk)
Injili ya Luka (Lk)
Injili ya Yohane (Injili ya Yohana) (Yn)
Matendo ya Mitume (Mdo)

Barua za Paulo[hariri | hariri chanzo]

Barua kwa Waroma (Waraka kwa Warumi) (Rum)
Barua ya Kwanza kwa Wakorintho (1 Kor)
Barua ya Pili kwa Wakorintho (2 Kor)
Barua kwa Wagalatia (Gal)
Barua kwa Waefeso (Efe)
Barua kwa Wafilipi (Flp)
Barua kwa Wakolosai (Kol)
Barua ya Kwanza kwa Wathesalonike (1 The)
Barua ya Pili kwa Wathesalonike (2 The)
Barua ya Kwanza kwa Timotheo (1 Tim)
Barua ya Pili kwa Timotheo (2 Tim)
Barua kwa Tito (Tit)
Barua kwa Filemoni (Flm)

Barua nyingine[hariri | hariri chanzo]

Barua kwa Waebrania (Ebr)
Barua ya Yakobo (Yak)
Barua ya Kwanza ya Petro (1 Pet)
Barua ya Pili ya Petro (2 Pet)
Barua ya Kwanza ya Yohane (1 Yoh)
Barua ya Pili ya Yohane (2 Yoh)
Barua ya Tatu ya Yohane (3 Yoh)
Barua ya Yuda (Yud)

Kitabu cha kinabii [5][hariri | hariri chanzo]

Ufunuo (Ufunuo wa Yohane) (Ufu)

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Biblia" ni neno lililoingizwa katika Kiswahili bila kutafsiriwa. Asili ya neno hili ni lugha ya Kiyunani. Tafsiri ya neno hilo ni "Vitabu" katika Kiswahili.
  2. Sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo inaitwa "Agano la Kale" kwa sababu inaeleza habari ya agano (mapatano) kati ya Mungu na wateule wake wa kale, Israeli
  3. Vitabu 27 vya mwisho vinaitwa hivyo kwa sababu vinaeleza habari ya agano (mapatano) jipya kati ya Mungu na wanadamu wote.
  4. Vitabu vinavyoeleza kuzaliwa, maisha, kazi, na kifo cha Yesu na mwanzo na kuenea kwa Kanisa kuanzia Yerusalemu hadi Roma.
  5. Kitabu chenye maelezo ya mambo yaliyokuwako, yaliyopo na yatakayokuwako.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Orodha ya vitabu vya Biblia kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.