Nyoka Mnafiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyoka mnafiki
Nyoka mnafiki wa Taita (Boulengerula taitanus)
Nyoka mnafiki wa Taita (Boulengerula taitanus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Amfibia (Wanyama wanaoanza maisha kwenye maji na kuendelea nchi kavu)
Oda: Gymnophiona (Nyoka wanafiki)
Ngazi za chini

Familia 10:

  • Caeciliidae
  • Chikilidae
  • Dermophiidae
  • Herpelidae
  • Ichthyophiidae
  • Indotyphlidae
  • Rhinatrematidae
  • Scolecomorphidae
  • Siphonopidae
  • Typhlonectidae

Nyoka wanafiki ni wanyama wa oda Gymnophiona katika ngeli Amfibia wafananao na nyoka au nyungunyungu wakubwa. Wanyama hawa si nyoka au nyungunyungu kwa ukweli na hata si Reptilia au Annelida. Wana mnasaba na salamanda na vyura lakini hawana miguu. Mkia wao ni mfupi sana au umetoweka, kwa hivyo kloaka iko karibu na mwisho wa mwili. Hupitisha maisha yao yote wakichimba ardhini lakini spishi za familia Typhlonectidae huishi majini na zina aina ya pezi juu ya sehemu ya nyuma ya mwili ambayo inazisaidia kwenda mbele majini. Macho ya nyoka wanafiki ni wadogo na yamefunika kwa ngozi. Kwa hivyo hawawezi kuona vizuri lakini wanaweza kutambua baina ya nuru na giza. Wanyama hawa wanatokea katika mahali pa majimaji pa tropiki kama Afrika, Asia ya Kusini-Mashariki na Amerika ya Kati na ya Kusini.

Kuzaa[hariri | hariri chanzo]

Nyoka wanafiki hawana ndubwi kama salamanda au vyura. Spishi chache tu (±25%) hutaga mayai, nyingine huzaa wana wanaofanana na wazazi wao. Hata watagamayai takriban wote hutoka mayai kama nyoka wadogo. Spishi chache tu zina wana wanaofanana na ndubwi wenye matamvua na hata hawa hawaishi majini lakini katika udongo chepechepe karibu na maji, isipokuwa wale wa Typhlonectidae.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]