Nyamtinga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyamtinga ni kata ya Wilaya ya Rorya katika Mkoa wa Mara, Tanzania yenye postikodi namba 31307.

Kata hiyo inapakana na kata ya Kirogo upande wa Kusini, Nyahongo upande wa Kaskazini Mashariki na ziwa Viktoria upande wa Magharibi.

Imeundwa na vijiji vinne yaani Nyarombo, Rwang'enyi, Busanga na Manila.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 14,008 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,203 waishio humo[2].

Kata hiyo ina shule takriban tano za msingi na shule moja ya sekondari. Mwamko wa elimu bado ni mdogo katika eneo hili, hasa kwa watoto wa kike ambao hukimbilia kuolewa punde tu wanapomaliza elimu ya msingi. Wengine huacha shule kabla ya kuhitimu. Hata wale wachache wanaofika Sekondari hawafanyi vizuri katika matokeo yao ya mwisho.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Rorya - Mkoa wa Mara - Tanzania

Baraki * Bukura * Bukwe * Goribe * Ikoma * Kigunga * Kinyenche * Kirogo * Kisumwa * Kitembe * Komuge * Koryo * Kyangasaga * Kyang'ombe * Mirare * Mkoma * Nyaburongo * Nyahongo * Nyamagaro * Nyamtinga * Nyamunga * Nyathorongo * Raranya * Rabour * Roche * Tai


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyamtinga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno.