Nyamera (jenasi)
| Nyamera | ||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nyamera wa kawaida
(Damaliscus korrigum jimela) |
||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Nyamera ni wanyamapori wakubwa wa jenasi Beatragus na Damaliscus katika familia Bovidae. Kwa asili jina hili lilitumika kwa nususpishi D. korrigum topi, lakini sikuhizi spishi na nususpishi zote huitwa nyamera mara nyingi. Majina mengine ni hirola, jimela, sasabi na tiang. Wanatokea savana za Afrika tu. Rangi yao ni ya mchangwa inayoelekea nyekundu au kijivu mara nyingi. Wana mabaka meusi mwilini, miguuni na kichwani, isipokuwa hirola, na nyamera baka-nyeupe ana baka nyeupe kwa pua na paji. Kichwa chao ni kirefu kama kile cha kongoni lakini pembe zao hazina umbo wa zeze. Wanyama hawa hula manyasi.
[hariri] Spishi
- Beatragus hunteri Hirola au Nyamera wa Hunter (Hirola au Hunter's Hartebeest)
- Damaliscus korrigum Nyamera (Topi)
- Damaliscus k. jimela Nyamera wa Kawaida au Jimela (Topi)
- Damaliscus k. korrigum Nyamera Magharibi (Korrigum)
- Damaliscus k. tiang Nyamera Kaskazi au Tiang (Tiang)
- Damaliscus k. topi Nyamera-pwani au Topi (Coastal Topi)
- Damaliscus lunatus Sasabi (Tsessebe)
- Damaliscus pygargus Nyamera Baka-jeupe (Bontebok)
- Damaliscus superstes Sasabi wa Bangweulu (Bangweulu Tsessebe)
[hariri] Picha
| Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyamera (jenasi) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.