Njia ya Pwani ya Welisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chepstow, njia inapoishia.
Mwanzo na mwisho wa Njia ya Pwani ya Welisi.

Njia ya Pwani ya Welisi (kwa Kiingereza: Wales Coast Path, kwa Kiwelisi: Llwybr Arfordir Cymru) ni njia ya matembezi marefu kwa miguu inayozunguka pwani yote ya Welisi. Njia inaanzia Queensferry, kaskazini mwa nchi ikiendelea hadi Chepstow (Kiwelisi: Cas-gwent) kusini mwa nchi.

Urefu wake ni kilometa 1,400.[1] Njia ilifunguliwa rasmi tarehe 5 Mei 2012, ila sehemu fulani kama Njia ya Pwani pa Ziwa ya Anglesey na Njia ya Pwani pa Pembrokeshire zilitanguliwa kufunguliwa. Njia inapitia Hifadhi za Taifa mbili, Maeneo Mazuri ya Urembo matatu na Hifadhi za Asili za Kitaifa 11.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. firstnature.com - Countdown to the Wales Coast Path Ilirejewa 10 Julai 2012.
  2. bbc.co.uk - Wales Coast Path officially opens with events in Cardiff, Aberystwyth and Flint Ilirejewa 10 Julai 2012.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]