Niger
Kwa maana nyingine ya neno "Niger" tazama makala ya Niger (maana)
|
|||||
| Wito la taifa: Fraternité, Travail, Progrès (Undugu, Kazi, Maendeleo) |
|||||
| Wimbo wa taifa: La Nigerienne | |||||
![]() |
|||||
| Mji mkuu | Niamey |
||||
| Mji mkubwa nchini | Niamey | ||||
| Lugha rasmi | Kifaransa | ||||
| Serikali | Jamhuri Tandja Mamadou Ali Badjo Gamatié |
||||
| Uhuru imetangazwa |
kutoka Ufaransa 3 Agosti 1960 |
||||
| Eneo - Jumla - Maji (%) |
1,267,000 km² (ya 22) 0.0002% |
||||
| Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
11,665,937 (ya 69) 9/km² (ya 175) |
||||
| Fedha | Franki ya CFA (XOF) |
||||
| Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+1) (UTC+2) |
||||
| Intaneti TLD | .ne | ||||
| Kodi ya simu | +227
- |
||||
Niger ni nchi ya Afrika ya Magharibi. Imepakana na Algeria na Libya upande wa kaskazini, Mali na Burkina Faso upande wa magharibi, Chad upande wa mashariki na Nigeria pamoja na Benin upande wa kusini. Mji mkuu ni Niamey katika kusini ya nchi.
Niger haina pwani na bahari yoyote. Ni sehemu ya kanda la Sahel yaani sehemu kubwa ya nchi ni yabisi, kaskazini yake ni yabisi sana ikiwa jangwa la Sahara, ardhi ya rutuba iko kusini kabisa karibu na mto wa Niger.
Mipaka imechorwa wakati wa ukoloni wa Ufaransa ikiunganisha watu wa utamaduni tofauti kama vile Watuareg wa Sahara, wahamiaji Wafulbe na Wakanuri wa eneo la Sahel na wakulima wa kusini kama Wasonghai na Wahausa. Angalia pia orodha ya lugha.
Tofauti hizi kubwa zilileta kipindi cha ugomvi wa makabila uliopoa tena baada ya mwaka 2000. Tatizo kubwa la nchi ni vipindi vya ukame na njaa vinavyorudia mara kwa mara.
Wakazi walikadiriwa kuwa karibu milioni 12 katika mwaka 2005. Idadi kubwa wako kusini. Walio wengi kabisa ni wafuasi wa Uislamu waliokadiriwa kuwa 94-97% za wananchi; sehemu yao wanasemekana kuchanganya Uislamu na imani asilia.
Viungo vya nje [hariri]
- (Kifaransa) Rais wa Niger tovuti rasmi
| Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Niger kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
| Nchi za Afrika | |
|---|---|
| Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
| Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
| Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia | |
