Nelly Sachs

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nelly Sachs (1910)

Nelly Leonie Sachs (10 Desemba 189112 Mei 1970) alikuwa mwandishi na mshairi Myahudi kutoka nchi ya Ujerumani. Mwaka wa 1940 alisaidiwa na rafiki yake Selma Lagerlof kukimbia ukatili wa WaNazi na kuhamia Sweden. Katika mashairi na tamthiliya zake alieleza mateso ya Wayahudi, k.m. katika tamthiliya "Eli: Juu ya Mateso ya Israel" (kwa Kijerumani Eli: Ein Mysterienspiel vom Leiden Israels) iliyotolewa mwaka wa 1951. Mwaka wa 1966, pamoja na Shmuel Yosef Agnon alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nelly Sachs kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.