Ndegejinga ni ndege wakubwa wa bahari wa familia Sulidae. Wana domo refu na mabawa marefu yaliyochongoka. Takriban spishi zote wana mwili mweupe na viasi mbalimbali vya nyeusi kwa mabawa na mkia. Spishi kadhaa zina namna kahawia na ndegejinga tumbo-jeupe ana rangi ya kahawa nzito na tumbo jeupe. Ndege hawa hupiga mbizi kutoka urefu kubwa ili kukamata samaki au ngisi. Huzaa ndani ya makoloni makubwa. Jike hutaga yai moja au mayai mawili, lakini kinda atokaye kwanza katika yai lake amsukuma ndugu wake mdogo nje ya tundu. Huyu afa kwa njaa au aliwa na ndege wa aina nyingine.
[hariri] Spishi za Afrika
[hariri] Spishi za mabara mengine
[hariri] Spishi za kabla ya historia
- Sula humeralis (kati ya Pliocene)
- Sula sulita (Peru, mwisho wa Miocene)
- Sula magna (Peru, mwisho wa Miocene/mwanzo wa Pliocene)
-
-
Koloni la ndegejinga kusi
-
-
-
Ndegejinga miguu-myekundu na tumbo-jeupe
-
Ndegejinga miguu-myekundu