Nathari
Nathari ni tawi moja la fasihi andishi. Tofauti na tenzi au ushairi unaoleta ujumbe wake kwa umbo ya mabeti nathari haina umbo maalumu au viwango vya muundo au taratibu. Hivyo inaweza kufanana na mazungumzo ya kila siku.
Nathari inafaa kwa habari na masimulizi. Inatumiwa kwenye magazeti, vitabu, jarida au kamusi.
Ni tungo za kisanii za kubuni ambazo hutumia lugha ya kimaelezo kimfululizo na kiinsha/mjazo kupasha ujumbe wa kuelimisha, kuburudisha. hujumuisha : riwaya,hadithi fupi, insha za kifasihi. TOFAUTI KATI YA NATHARI NA USHAIRI
Marejeo[hariri]
Wamitila, K.W. 2003. Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia, Nairobi: Focus Books.
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.