Natalie Grant
| Natalie Grant | |
|---|---|
| Maelezo ya awali | |
| Jina la kuzaliwa | Natalie Grant |
| Amezaliwa | 21 Desemba 1971 Seattle, Washington |
| Aina ya muziki | Nyimbo za kisasa za Kikristo |
| Kazi yake | Mwanamuziki na Mtunzi wa Nyimbo |
| Ala | Sauti |
| Miaka ya kazi | 1999 hadi sasa |
| Studio | Curb Records |
| Tovuti | Tovuti Rasmi |
Natalie Grant (amezaliwa tar. 21 Desemba 1971, mjini Seattle, Washington) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za kisasa za Kikristo. Kazi yake imepata umaarufu, pamoja na tuzo nne mfululizo za Dove Awards za mwanamuziki bora sana kwa wanawake, na kwa wimbo wake uliojulikana sana, "Held". Aliyezaliwa mjini Seattle,yeye sasa anaishi Nashville na mumewe, Bernie Herms. Alituzwa na Muungano wa Nyimbo za Kikristo tuzo ya Mwimbaji wa kike wa Mwaka katika miaka ya 2006, 2007, 2008 na 2009.
Yaliyomo |
Wasifu [hariri]
Maisha ya awali [hariri]
Natalie aliolewa na mzalishaji wa muziki Bernie Herms na alijifungua mapacha wasichana, Grace Ana na Isabella Noelle, tarehe 16 Februari 2007. Alikuwa msemaji na mtendaji kwenye ziara ya Revolve, mkutano kwa wasichana waliobaleghe ulioandaliwa na Wanawake wa Imani.
Albamu yake ya saba, Relentless, ilitolewa tarehe 12 Februari 2008. Vibao kadhaa kutoka albamu hii mpya viliimbwa katika ziara ya Revolve.
Alizuru hivi majuzi kwa ziara ya Speaking Louder Than Before akiwa pamoja na Bebo Norman na Jeremy Camp.
Diskografia [hariri]
Albamu [hariri]
- Natalie Grant (1999)
- Stronger (2001)
- Deeper Life (2003)
- Worship with Natalie Grant and Friends (2004)
- Awaken (2005)
- Believe (2005)
- Relentless (2008)
Makala ya Waandishi [hariri]
- The Real Me: Being the Girl God Sees ISBN 0849908825
Tuzo [hariri]
Tuzo za GMA Dove [hariri]
- 2006: Mwimbaji wa kike wa mwaka.
- 2007: Mwimbaji wa kike wa mwaka.
- 2008: Mwimbaji wa kike wa mwaka.
- 2009: Mwimbaji wa kike wa mwaka.
Marejeo [hariri]
1 ^ "GOSPEL MUSIC ASSOCIATION ANNOUNCES INITIAL HOSTS AND PERFORMERS FOR 41st ANNUAL DOVE AWARDS, TO BE HELD ON APRIL 21, 2010 AT NASHVILLE'S FAMED GRAND OLE OPRY® HOUSE". gospelmusic.org. 2009-12-23. http://www.gospelmusic.org/newsmedia/pressRoom_detail.aspx?iid=42151&tid=33.
2 ^ "Twins for Natalie". crossRhythms.co.uk. 2007-03-01. http://www.crossrhythms.co.uk/articles/news/Twins_For_Natalie/26341/p1/.
3 ^ "Shine FM::Matukio". 951shinefm.com. 2010-01-08. http://www.951shinefm.com/Dynamic/DynCon.aspx?cid=52&lpk=262.
Viungo vya nje [hariri]
- Tovuti rasmi ya Natalie Grant
- Video ya Natalie kwa tovuti ya YouTube