Nakheel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nakheel PJSC
AinaKampuni inayomilikiwa na Serikali
Ilipoanzishwa2000
Makao MakuuDubai, United Arab Emirates
Eneo linalohudumiwanchi 87
Watu wakuuSultan Ahmed bin Sulayem (Mwenyekiti mkuu), Chris O'Donnell (CEO )
Sektamali isiyohamishika
Wafanyakazi2000

Nakheel (kwa Kiarabu: mitende) ni kampuni inayoshughulika na mali isiyohamishika iliyo na makao yake Dubai na imeumba miradi kadhaa inayohusika na kurejesha ardhi, ikiwemo Palm Islands, Dubai Waterfront, Visiwa vya The World na Visiwa vya The Universe. Miradi yake ya makazi yake ni pamoja na The Gardens, International City, Visiwa vya Jumeirah na Jumeirah Lake Towers. Miradi yake ya majumba ya ununuzi ni pamoja na Dragon Mart (katika International City) na Ibn Battuta Mall. Mshindani wake mkuu katika ujenzi wa majengo ya makazi Dubai ni Emaar Properties.

Mradi mashuhuri zaidi wa Nakheel ni ujenzi wa visiwa vitatu vilivyoundwa na binadamu vyenye umbo la mti wa mitende kwenye pwani ya Dubai. Nakheel inafanya kazi chini ya mwavuli wa Dubai World, ambayo husimamia biashara mbalimbali kwa niaba ya serikali ya Dubai. Mwenyekiti mtendaji wa Al Nakheel ni Sultan Ahmed bin Sulayem.

Miradi ya Nakheel ya mali isiyohamishikani pamoja na Palm Islands (Palm Jumeirah, Palm Jebel Ali, Palm Deira), Visiwa vya The World, Visiwa vya The Universe, Dubai Waterfront, The Gardens, Jumeirah Lake Towers, Discovery Gardens, Lost City, Visiwa vya Jumeirah, Jumeirah Heights (manyumba ya makazi ndani ya visiwa vya Jumeirah), Kijiji cha Jumeirah, Bustani ya Jumeirah, Al Furjan, International City, Jewel of the Palm, The Golden Mile (ambayo iko katika shina la Palm Jumeirah), Hoteli ya Kimataifa ya Nakheel, mradi mwingine katika shina la Palm Jumeirah, na Ibn Battuta Mall.

Nakheel imetangaza mipango ya ujenvi wa Nakheel Tower, ambayo itakuwa jengo refu zaidi duniani baada ya kujengwa, ikisimama juu ya theluthi mbili za maili kwenda juu. Jengo hili litachukua zaidi ya miaka 10 kukamilika na itakuwa katikati ya eneo kubwa la maendeleo, Bandari ya Nakheel. Mapema mwaka 2009 ujenzi ulisimamishwa kutokana na madhara ya umaskini duniani.

Inamiliki pia Meli ya kifahari ya kitambo ya, Queen Elizabeth 2, ambayo wanapanga kulibadili katika hoteli ya anasa, ambayo ingewekwa katika Palm Jumeirah lakini sasa itatumiwa kwa mradi wa DP Dunia mjini Cape Town, Afrika ya Kusini.

Tarehe 25 Novemba 2009, serikali ya Dubai ilitangaza kuwa Dubai World ilipanga "kuuliza wadhamini wote wa fedha kwa Dubai World na Nakheel 'wasimame' na kuongeza muda wa deni mpaka 30 Mei 2010".

Tarehe 14 Desemba 2009, serikali ya Dubai ilipokea $ bilioni 10 ya misaada kutoka kwa Abu Dhabi kwa Dubai World,iliyokuwa na madeni chungu nzima, ambayo ilisema itatumia $ dola bilioni 4.1 kwa kulipia deni ya Nakheel iliyokuwa ikifika tarehe ya malipo siku iyo hiyo. [1]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Picha mbalimbali

Picha za hewani ya Discovery Gardens tarehe 1 Mei 2007

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nakheel kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.