Muungano wa Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Muungano wa Afrika ni jina la harakati iliyolenga kuunganisha watu wote Waafrika au wenye asili ya Afrika kote duniani. Ha ni pamoja na wakazi wa Afrika wenyewe na wakazi wenye asili ya Kiafrika katika nchi za Amerika ambao mababu walipelekwa huko kama wafungwa wakiuzwa katika biashara ya watumwa.

Mara nyingi maslahi ya watu weusi ambao ni wakazi asilia wa Melanesia ya Pasifiki walihesabiwa humo.

Harakati ilianza kama harakati ya kiutamaduni ikaendelea kuwa harakati ya kisiasa iliyotaka kuunganisha nchi huru za Afrika baada ya mwisho wa ukoloni kwa lengo la kutengeneza nchi moja yenye serikali moja.

Wazo hili lilianza kipindi cha mapambano ya kupigania haki za waafrika dunia nzima, mapambano haya yaliungwa mkono na wanaharakati kama vile Marcus Garvey, William E. B. Du Bois ambao waliishi Marekani na Kwame Nkrumah wa Ghana na Julius Nyerere wa Tanzania. Harakati hizi zilianzia nje ya Afrika kwa kuwapigania waafrika walioteswa kama watumwa hasa Marekani, harakati hizo zilienea hadi Afrika ambapo mkutano wakwanza ulifanyikia Ghana katika mji mkuu wake Accra. Mara tu baada ya Ghana kupata uhuru mwaka 1957, mwaka 1958 raisi wa Ghana Kwame Nkrumah alitoa wazo la kuunda umoja wa afrika.

Baada ya mazungumzo marefu wazo hilo lilikubaliwa na viongozi wa nchi huru za kiafrika akiwemo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania. Hivyo basi umoja wa afrika OAU ambao sasa unaitwa AU uliundwa mwaka 1963 nchini Ethiopia iliyokuwa nchi ya pekee ya Afrika ambayo ilifaulu kujitetea dhidi ya uenezaji wa koloni katika karne ya 19. Addis Ababa ndipo makao makuu yake. Nyerere na Nkrumah walifikiri zaidi ni kwa vipi bara la Afrika lingeungana.

Nyerere na mwenzake Brazaville na kikundi cha monrovia walitaka hatua hizo zakutengeneza nchi moja ya afrika zisiharakishwe,Nyerere alitoa mawazo ambayomkwake yeye aliona yasinge ruhusu muungano wa haraka kama alivyo taka Nkrumah

Alisema kila nchi inayo haki yta kutengeneza uchumi na siasa yake ili kuifanya nchi hiyo kuambulika,lugha na tamaduni zake pia zingestahiri kutambulisha nchi hizo.Hivyo basi alisema nivigumu kuwaunganisha watu wente tamaduni tofauti lazima kwanza tofauti hizo za kitamaduni ziondolewe kitu ambacho kilihitaji mudazaidi.

Pia alisema matatizo mbalimbali yanayo zikumba nchi za kiafrika yakiwemo umasikinilk,vita vya wenyewe kwa wenyewe ujinga na magonjwa mbalimali pia njia tofautitofauti za utawala wqa viongozi vingekuwa vikwazo kikubwa cha kuunda umoja huo

Nyerere alitoa wazo la kuunda mashirika mbalimbali yanayo ziunganisha nchi zakiafrika kwanza kama hatua mojawapo ya kuelekea kuunda afrika moja,hivyo mashirika kama vila SADAC, ECOWAS,COMESA,EAC nakadhalika yaliundwa.

Nae Nkrumah alikuwa na mawazo kadha wa kadha ambayo kwa kiasi fulani yalitofautiana na yale ya nyerere kama vile;

Nkrumah na wenzake kutoka nchi za Mali,Nigeria, na Guinea wlitaka kuharakishwa kwa umoja huo vinginevyo waliona kuwa ni kupoteza muda.Nkrumah alisema haya kwa vigezo vifuatavyo;

Kuundwa kwa umoja wa afrika hakuwzi kuzifanya nchi zikose uhuru bali itasaidia kuleta muungano baina ya waafrika wenyewe,pia aliendelea kusema tatizo la tamaduni tofauti halikustahiri kukwamisha harakati za kuunda umoja wa afrika kwani kuendelea kuchelewa kunge toa nafasi kwa wakoloni kurudi kuitawala afrika kwa urahisi hivyo umoja ilikuwa njia pekee ya kuwazuia wakoloni kututawala tena na hayo matatizo mengine mengi yangeendelea kutatuliwa huku umoja ukiwa umesha undwa.

Nkrumah pia alisema muungano wa afrika ungesababisha kujenga nchi huru na imara yanye kusimamia maamuzi yake dhidi ya uzalishaji katika kilimo na bei katika soko la dunia ambayo ilimilikiwa na kupangwa na mabepari.

Kwa kuangalia na kutathimini mawazo haya viongozi hawa walionekana kuwa chumvi ya afrika kwa msaada wao katitika kujenga na kuleta uhuru miongoni mwa nchi za afrika

Kwa kuhitimisha, viongozi hawa,Nkrumah,Nyerere na wengineo kama vile Jomo Kenyatta wa Kenya, Kamuzu Banda wa malawi na Nelson Mandela wa Afrika Kusini ni miongoni mwa viongozi wa afrika wanao stahili kukumbukwa kwa mchango wao mkubwa katika kupigania uhuru wa afrika.Kategorie:Politik (Afrika) Kategorie:Geschichte (Afrika) Kategorie:Nationalismus