Musikari Kombo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Faili:Musikari Kombo.jpg
N. Musikari Kombo

Musikari Nazi Kombo (alizaliwa mnamo 13 Machi 1944 katika wilaya ya Bungoma) ni mwanasiasa kutoka nchi ya Kenya na sasa anahudumu kama Mbunge wa kuteuliwa. Alijiunga na Shule ya Msingi ya Misikhu kwa elimu yake ya msingi, kisha akajiunga na shule ya msingi ya Rakwaro, na hatimaye kuhamia Mumias ambapo yeye alimaliza elimu ya msingi. Kisha alijiunga Shule ya Upili ya Nyeri High School kwa elimu yake ya sekondari.

Alisomea masomo yake ya shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Nairobi na somo lake kuu lilikuwa somo la Kiuchumi. Awali aliuwa anaiwakilishwa eneo bunge la Webuye, kwanza baada ya kuchaguliwa ofisini mwaka wa 1992. Pia aliwahi kuhudumu katika Serikali ya Kenya kama naibu waziri wa Mipango na Waziri wa Maendeleo ya Mkoa. Alichukua ofisi ya Wizara ya serikali ya Mtaa, mwishoni mwa mwaka wa 2003. Kombo kwa sasa ni Mwenyekiti wa chama cha FORD-Kenya.

Hivi sasa, yeye ni mbunge wa zamani wa Webuye baada ya kupoteza kiti chake kwa mgombea wa Orange Democratic Movement (ODM), Alfred Sambu katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya wa mwaka wa 2007.

Anakotoka Kombo[hariri | hariri chanzo]

Musikari Kombo anatoka katika jamii ya Kibalunda ambayo ni sehemu ndogo ya kabila ya Kibukusu ambayo pia ni sehemu ndogo ya jamii kubwa ya Waluhya. (ukoo wa Mulunda, unaaminika kuhamia nchini Kongo kutoka Afrika Mashariki).

Yeye ni Katoliki na dini.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]