Eneo bunge la Mugirango Kaskazini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mugirango Kaskazini)
Jamhuri ya Kenya

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Kenya



Nchi zingine · Atlasi


Eneo bunge la Mugirango Kaskazini ni moja ya Majimbo ya Uchaguzi ya Kenya linalopatikana katika Kaunti ya Nyamira.

Idadi ya Wapiga Kura[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 1999, Jimbo hili lilikuwa na jumla ya watu 156,344, 89092 kati yao wakiwa wamejiandikisha kupiga kura mnamo 2007.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Awali, eneo la Mugirango Kaskazini lilikuwa eneo moja kubwa. Mnamo 1966, jimbo hili liligawanya na kuwa Mugirango Magharibi na Mugirango Kaskazini iliyopungua. Jina lake lilibadilishwa mnamo 1974 na kuwa Borabu / Mugirango Kaskazini, ambalo mwishowe lilibadilishwa kuwa Mugirango Kaskazini / Borabu mnamo 1986.

Wilfred Moriasi Ombui[1] alikishinda kiti hiki katika Uchaguzi wa 2007 huku akimshinda mpinzani wake Godfrey Masanya Okeri ambaye ndiye aliyekuwa Mbunge kati ya 2002 na 2007[2].

Wadi za Kupiga Kura[hariri | hariri chanzo]

Wodi ziundazo Mugirango Kaskazini ni: Ekerenyo, North Mugirango Chache, Bomwagamo, Kiabonyoru, Kiangeni, Makenene, Nyansiongo na Esise.

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Maendeleo Afrika,www.afdevinfo.com Archived 13 Desemba 2009 at the Wayback Machine.
  2. Ripoti ya Maendeleo ya Afrika www.afdevinfo.org Archived 3 Julai 2009 at the Wayback Machine.