Mtumiaji:Kipala/Archive 6

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Archive Hii ni ukurasa wa Hifadhi ya Majadiliano ya Awali. Usihariri ukurasa huu usiongeze wala kupunguza kitu.
Ukitaka kujadiliana upya mambo yaliyomo humo nenda kwa ukurasa wa majadiliano ya sasa.


Mbegu za jiografia ya Tanzania

Kipala, salam. Nimejaribu kuumba Kigezo:Tanzania-geo-stub ambayo ndani yake imeambatana na JAMII Jamii:Mbegu za jiografia ya Tanzania, nikiwa na lengo la kutumia kigezo bila kuweka jamii, yaani ijiweke jamii yenyewe kama jinsi ilivyo ile ya"MBEGU". Je, unaweza kuitazama kwanini ile haitaki kujumuisha makala kwenye jamii ile ya Mbegu za jiografia ya Tanzania?--Mwanaharakati (Longa) 12:10, 18 Desemba 2008 (UTC)

Je ni hii unayotaka? Nimenakili maandiko ya "mbegu". Halafu: je si afadhali makala yote ya Dar yaingie jamii:Dar es Salaam? --Kipala (majadiliano) 12:25, 18 Desemba 2008 (UTC)
Suala si kuichukua ile ya "mbegu", la. Ninachotaka pale unapoweka hiki kigezo cha Tanzania-geo-stub JAMII ijiweke yenyewe kama jinsi ilivyoelekwa kile kigezo cha "mbegu". Labda uuangalie tena namna ilivyo hii ya "mbegu" na hii mpya.--Mwanaharakati (Longa) 12:33, 18 Desemba 2008 (UTC)
Nisipokei inafanya hivyo angalia jamii:Mbegu za jiografia ya Tanzania makala nyingi zimo. Ila tu haionyeshi chini kwenye ukurasa. --Kipala (majadiliano) 15:44, 18 Desemba 2008 (UTC)
BAsi tatizo limekwisha. Ilikuwa neno "jamii" badala ya "category". Kumbe kutafsiri meta kuna mambo mengi.--Kipala (majadiliano) 15:54, 18 Desemba 2008 (UTC)
Sidhani kama hilo lilikuwa ndilo tatizo. Sasa hivi hata ukiweka JAMII AU CATEGORY zote zinafanya kazi moja! Awali tulikuwa hatuna muundo wa kutaja "JAMII" ila kwa sasa nasi tunao!! Hivyo si lazima kuweka CATEGORY katika makala kwani hata JAMII yaweze kutoa huduma hitajifu. Ninashukuru kwa ushirikiano wako mzee wangu. Na kwa sasa ninafanya ile kazi uliyonitaka nifanye ya kuandika japo kidogo miji ya kwetu. Nimeshaanza tayari..--Mwanaharakati (Longa) 16:07, 18 Desemba 2008 (UTC)
Nimefurahia sana kuona makala hizi! Hata hivyo bado naona tatizo ni jamii/category kwa sababu sasa inaonyesha nadhani kuna mahali pawili au zaidi ambako kunahitaji kubadilishwa na si rahisi kupata kote.--Kipala (majadiliano) 17:25, 18 Desemba 2008 (UTC)

Ni kweli usemavyo, lakini hili unalolisema ninahisi nalifahamu! Yaani hata kama kwa ndani tunatumia neno Jamii:fulani... Lakini bado kwa nje inataja vilevile CATEGORY au CATEGORIES, sio? Nalo tayari ishabadilishwa! Kama unakumbuka kule kwenye kona ya majadiliano nilikuwa nikikuuliza kuhusiana na "mfumo wa jamii" nawe hukunitupa mkono na kwa pamoja tulifanikiwa kubadilisha CATEGORY TREE kuja "MFUMO WA JAMIII". Kingine: Hata ukibadilisha zile ujumbe bado yule msimamizi wa kule atafanya kwa wakati wake (hiyo ni kwa mujibu wa FAQ za BetaWiki!). Hivyo hata ile CATEGORY ya nje kwenye kiungo onyeshi itabadilika pindi yeye atapoiweka kwenye MediaWiki kuu! Tuendeleze wiki yetu..--Mwanaharakati (Longa) 05:14, 19 Desemba 2008 (UTC)


Kipala, salam! Naomba utazame swali langu hapa!--Mwanaharakati (Longa) 12:04, 19 Desemba 2008 (UTC)

Hongera ya makala 8,000

Jamani tumefikia makala 8,000 Naona mzee wangu ulichapa kazi kwa kiasi kikubwa kabisa katika siku mbili tatu zilizopita. Na hizo ndizo zilizopelekea kuwa na kiwango hiki Ka! Nahisi kupumua kidogo kwa kufuatia mfululizo wa makala za hapa na pale tulizochangia hapa mwetu. Zaidi na zaidi ni kukupongeza kwa kazi yako! Basi tuendelee kushauriana na kuvumiliana!!!!--Mwanaharakati (Longa) 14:37, 19 Desemba 2008 (UTC)

Kipala, salaaam! Eh, ni kweli kuhusiana na kuongezea nyama katika mifupa! Huruma ni kwamba sijui mengi kuhusiana na miji hii ya kwetu, hivyo nitajitahidi kuisoma katika makala za mitandao mingine! Kingine, labda nikupe hongera ya endelezo lako la makala za msingi zile za orodha ya meta! Kwani ukimaliza nasi tutakuwa wamoja kati ya waliotii mfululizo ule!! Ubarikiwe--Mwanaharakati (Longa) 05:44, 20 Desemba 2008 (UTC)

Mbegu za jiografia ya Tanzania - mpya

Kipala, salam na kheri ya mwaka mpya! Kwa sasa ninataka niendeleze ile mbegu ya kata na wilaya za Tanzania, lakini bado najifikiria kuhusu ile hali yake ya kuwa mifupa mitupu! Je, inafaa kuendeleza orodha ile hadi kufikia hatua ya kumaliza orodha ile, au niishie pale tu nilipofikia kwa kufuatia uhaba wa maelezo zaidi?--Mwanaharakati (Longa) 05:59, 6 Januari 2009 (UTC)

Asante kwa swali. Mimi naona ya kwamba mbegu hizi zina maana. Ni mwaliko kwa watu wengine kuongeza habari fupifupi. Naona ya kwamba sehemu kubwa ya mbegu hizi itabaki kama "kiunzi cha mifupa tu" lakini ni rahisi zaidi kuongeza kitu mara mbegu ipo. Mimi nitafurahi ukiendelea. --Kipala (majadiliano) 09:28, 6 Januari 2009 (UTC)
Kipala, salam! Nimeona ukiandika mengi kuhusu miji na kata zile ulizokuwa ukiishi hapo awali. Ni furaha iliyoje kuona miji ile ya kwetu ikiandikwa na wewe. Pia nimepta kujifunza kitu kimoja ambacho awali sikuwa na nfanya. Kuweka JAMII Kata za Wilaya fulani! Nilikuwa nikiweka mji wake bila JAMII zake! Basi endelea na hiyo miji huku nikiwa nakili kama ninajifunza kupita kwako! Kila la kheri! --Mwanaharakati (Longa) 08:46, 10 Januari 2009 (UTC)

Jamii - Kata

Aha, kwa hiyo kila wilaya iwe na JAMII ya kata zake, si ndiyvyo? Maana yake kata zote awali nilikuwa nikiziweka kwenye mkoa wake. Kwa mfano: Kata ya Kiwalani, Tabata, Mwenge, n.k... Nimeziweka zote kwenye JAMII ya Dar es Salaam kwa mujibu wa maelezo yako ya awali. Ama unataka vipi hapo?--Mwanaharakati (Longa) 13:19, 10 Januari 2009 (UTC)


Salaaam! Kwanza samahani kwa kuchelewa kukujibu, kwani huku kwetu kulikuwa na Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar! Hivyo sikuweza kuja kazini kwa siku ya Jumatatu na Jumapili kama ilivyoada! Haya, hongera zote zirudi kwako kwa kutoa wazo la kuanzisha makala hizi, kwani mie mwenyewe sikuwa na wazo la karibu kufikia kuandika makala za miji ya kwetu! Hivyo hongera nawe! KUHUSU KATA NA JAMII: Naunga mkono hoja la kuweka JAMII husika katika kila Wilaya kuliko zote kuziweka kwenye JAMII ya mkoa wake. Hivyo kutoka sasa tutahitajika kuumba JAMII kwa kila mkoa tutakao amia! Lakini hapa bado nina sawali moja: JAMII za chini zitaitwaje? Yaani endapo tutaanzisha JAMII:KATA ZA WILAYA YA MBOZI - kwa mfano, jamii ya chini itakuwa ipi?--Mwanaharakati (Longa) 06:21, 13 Januari 2009 (UTC)
Sijui kama tutazihitaji. Itategemea.
  • Kwanza naona ukubwa wa jamii. Kama inadikia makala 100 ukurasa hausomeki tena kirahisi, lazima kusukuma makala katika jamii za chini.
  • Halafu ni swali la kupanga makala kwa upatikanaji. Yaani kama nchi fulani ina makala 5 tu (nchi, mji mkuu, mto mmoja, mwanasiasa mmoja, nchi ya kihistoria ndani yake) naona ni vema kuweka kila makala katika jamii mbili: upande mmoja kwenye nchi, upande mmoja kwenye kundi lake kama miji mikuu n.k. . Ndani ya nchi sioni faida ya kupanga mji 1 au 2 katika jamii "miji ya XYZ" kama ni chache sana tu (ingawa nimeshafanya hivyo awali).
  • Kwa Wilaya hadi sasa naona jamii 1 inatosha tuweke kata na kila kitu ndani yake "Jamii:Wilaya ya XYZ"--Kipala (majadiliano) 07:53, 13 Januari 2009 (UTC)
Tupo pamoja mzee wangu. Lakini bado nina swali moja: Vipi kuhusu ile jamii ya "MBEGU ZA JIOGRAFIA YA TANZANIA" naona ina jumlisha makala zooote tutakazoumba kwa kufuatia kile kigezo cha "TANZANIA-GEO-STUB" imewezesha kuweka JAMII ile bila sisi kuandika chochote ina yenyewe itajaza makala tajwa. Inakuwaje?--Mwanaharakati (Longa) 14:59, 13 Januari 2009 (UTC)

Kata

Sijambo, Kipala. Ni kweli. Lakini safari hii sijakulupuka kama nilivyofanya awali kwenye Wilaya moja hivi. Na pia, bado ninafuata ule utaratibu uliousema wa kutumia jina la kata (kwa wilaya yake) na sio "kata." Ninashukuru kwa ushauri wako na bado nitaendelea kuusikiliza na kuufuata ushauri wako! Kila la kheri!--Mwanaharakati (Longa) 09:55, 17 Januari 2009 (UTC)

Naomba msaada. Nataka kujua maana ya maneno haya:
  • "Knowledge Reigns Supreme Over Nearly Everyone."

Nitashukuru ukinipa maana hiyo!--Mwanaharakati (Longa) 13:26, 17 Januari 2009 (UTC)

Elimu/Akili/Utaalamu hushinda karibu watu wote - kwa Kiswahili lazima kuamua unataka kuweka uzito upande gani. --Kipala (majadiliano) 15:24, 17 Januari 2009 (UTC)


mwanafunzi wa kutunga makala

Ni mwanafunzi mpya wa kutunza makala yenye lugha hii nzuri na mpya kabisa kutangaza kwenye wikipedia. Hivyo usiwe na matazamio mengi juu yangu hasa kuhusu matangazo, ila mtu abarikiwe awezeye kunizaidia jinsi ya kutangaza ama kurekebisha makala ambazo nimetunga. Ninatumia jina la Rehema nikiwa ndani hapa na makala ya kwanza ambayo nimezaidia kutunga ni juu ya hilo jambo "figo". Kama mwanafunzi wa mambo ya uuguzi nina moyo na upendo kupanusha ujuzi juu ya mambo ya mwili, maradhi na mengineyo.

-Rehema 2009/01/18 imeandikwa na user:rehema

Karibu sana dada (au: ndugu?) Rehema! Ikiwezekana naomba uchukue hatua ya kujiandikisha na kufungua ukurasa wako. Unafika ukibonyeza "sajili akaunti" kwenye kona ya juu. Hapa unapata chaguo la kujiandikisha kwenye dirisha la "Ingia - sajili akaunti". Faida yake ni ukiingia na kufanya log-in utaona mara moja kama mtu ameandika kitu kwenye ukurasa wako; pia unapewa nafasi ya kutazama makala ulizoteua. Kuhsu "figo" nina mapendekezo kadhaa lakini sasa nina kazi nyingi kidogo siku zinazozokuja. --Kipala (majadiliano) 18:08, 18 Januari 2009 (UTC)
Ahsante kwa tafsiri yako ya juu! Halafu, nina nakili maelezo yako ya majibu ya huyu dada na kuyapeleka kule kwenye ukurasa wake wa majadiliano. Akiwa bado ni mgeni na zana hizi, sizani kama atakuwa na uwezo wa kufikiria haraka ya kujua kama swali lake limejibiwa! Ninatanguliza samahani kwa tukio hili. --Mwanaharakati (Longa) 07:18, 19 Januari 2009 (UTC)

hongera na pole

Bwana, kazi nyingi naiona unayoifanya. Hongera! Na pole vilevile. Wako katika enezi la lugha yetu pendwa, --Baba Tabita (majadiliano) 09:18, 28 Januari 2009 (UTC)

Asante. Natumaini ya kwamba mbegu wa kijiji utavuta watu kuongeza ya kwao; nimeshaiona mara chache. --Kipala (majadiliano) 10:13, 28 Januari 2009 (UTC)

Vigezo

Kipala, salam! Sasa nimeshaanza na hii. Lakini naona hujaendeleza ile Wilaya iliyofuata. Nilifikiri ya kwamba unaumba vigezo vya Mkoa mzima wa Mbeya! Lakini si kitu. Baadaye kama utapata muda, basi naomba malizia vigezo vya wilaya zote za Mbeya! Huku mimi nikiwa nahamie mjini Morogoro kwa fujo zaidi. Je, wewe umeshaanza kuandika kata yoyote ya wilaya ya mkoa huo? (Morogoro)--Mwanaharakati (Longa) 13:42, 28 Januari 2009 (UTC)

Muddy, pole na usumbufu, sasa vigezo vyote vya mkoa wa Mbeya tayari nisipokosei. Mkoa wa Morogoro pia (nadhani, ilikuwa kazi ya usiku). Iringa kata ziko tayari isipokuwa Iringa mjini. --Kipala (majadiliano) 14:17, 28 Januari 2009 (UTC)
Ahsante kwa pole mzee wangu. Basi unastahili hongera (hadi usiku hufanya shughuli za wiki?) Mie sasa naona nina nafuu kiasi hata niweze kumaliza mikoa hiyo kwa chapchap. Kingine ni kufurahi kwa wawili sisi kuvunja rekodi ya ongezeko la makala za wiki (elfu kwenda elfu) kwa mara moja hivi! Eti hadi sasa tupo na makala 79,947 katika Wikipedia hii, wakati juzijuzi tu, tumefikisha elfu nane! Je, hatuwezi kutoast?? --Mwanaharakati (Longa) 15:31, 28 Januari 2009 (UTC)

Translation

Please, could you translate this article onto Swahili language? Thanks a lot for your help. If you want to translate any article onto Galician, Catalonian, Spanish or Portuguese, tell it to me.--Chabi

Hongera ya makala 9,000

Kipala, salam. Ni siku 43 nyuma, yaani, 19 Desemba 2008 hadi tar. 2 Februari 2009 - 9,000. Leo tuna makala 9,000. Inazidi kuifanya Wikipedia yetu kuwa vilevile ya pili kama jinsi ilivyozoeleka! Sina maneno mengi, ila ni kukutakia furaha ya kufika hapa tulipo! Pia, maisha mema na kazi kwa ujumla. Kila la kheri. --Mwanaharakati (Longa) 16:02, 2 Februari 2009 (UTC)

Kata na uchovu!

Kipala, salaaaam! Mzee wangu we, sijui hata ilikuwaje. Labda kweli huenda ikawa uchovu hadi kupelekea kusahau kubadili mkoa husika. Ninashukuru kwa kutotiwa nguvuni kwa kosa la kuhamisha mkoa wa rais na bunge lake Pia, ninashukuru kwa masahihisho uliyoyafanya kwenye kurasa zote zilizokosewa! Basi tuvumiliane hivyohivyo mzee wangu. Kazi njema.--Mwanaharakati (Longa) 07:19, 10 Februari 2009 (UTC)

Mkoa wa Kilimanjaro

Kipala, salaam! Nimeshaanza na tajwa hapo juu. Lakini naanza tu, nakuta Wilaya Rombo haina kigezo kama jinsi ilivyoada! Sikufanya hajizi nami nikaumba kigezo chake. Je, ni Mkoa mzima hauna vigezo ama Wilaya moja tu? Ninafuata utaratibu ule ulioweka kule kwenye Makabadiliko ya Hivi Karibuni! Basi naomba niangalizie kama vigezo vyote vya Mkoa huu kama vipo tayari, ikiwa bado basi nitaviweka halafu baadaye nivianzishie makala! Kazi njema.--Mwanaharakati (Longa) 10:03, 12 Februari 2009 (UTC)

Kweli Kilimanjaro utaona zaidi orodha ya kata kuliko kigezo. Kwa kazi ya kata haina tofauti. Weka tu nafasi ya Kigezo:Kata za wilaya ya Rombo na kadhalika nitaishughulika mwenyewe au fanya wewe kwa sababu si kazi kubwa (kunakili majina ya kata kutoka dirisha la hariri kwenda word, katika word search/replace "^p" kwenda " | " na kuingiza katika fomu ya kigezo. Ila tu naweza kuifanya baadaye. --Kipala (majadiliano) 10:07, 12 Februari 2009 (UTC)
Basi nitasubiri hadi hapo utakapoiumba!--Mwanaharakati (Longa) 11:33, 12 Februari 2009 (UTC)
Mkoa wa Kilimanjaro ushafanyika! Naomba mzee wangu unisaidie japo kuhamisha kule kwenye mabadiliko ya karibubuni, tafadhali. Ninajisikia nimechoka baada ya kumaliza mkoa huo. Basi sasa naenda nyumbani - Mungu akijalia kesho nitaendeleza hiyo miji mingine! Kazi njema.--Mwanaharakati (Longa) 15:45, 12 Februari 2009 (UTC)

Austistic - Autism

Kipala, salam. Naomba nisaidie kuelewa ugonjwa? Huo niliyoutaja hapo juu. Shida ni kwamba, siambui kwa Kiswahili vizuri! Sasa naomba unifafanulie namna ya haya majina ya Austistic au Autism. Kazi njema.--Mwanaharakati (Longa) 14:05, 13 Februari 2009 (UTC)

Mzee wangu, pole na kazi. Ukiona umepata muda wa kutosha kiasi hata kuweza kulijibu ombi la swali langu hapo juu, nitashukuru! Basi ni hayo tu, mzee wangu.--Mwanaharakati (Longa) 13:39, 19 Februari 2009 (UTC)
Nisamehe basi nitajaribu kujibu. Hii ni ama ugonjwa au hali ya pekee ya akili ya mtu. Inaanza kuonekana kwa watoto wadogo. Mtu anayeathiriwa nayo hawasiliani na watu wengine kama "watu wa kawaida". Hii ni sababu ya jina linalomaanisha "mtu wa pekee, mtu anayekaa ndani yake mwenyewe". Watu hao wanasemekana wana matata ya pekee na pia wanaweza na nguvu za pekee. Kati ya matata ni ya kwamba hawawezi kusoma uso wa mtu hawatazami macho si wanashindwa kuelewa jinsi gani mtu anajisikia kama anaonyesha furaha, hofu au wasiwasi. Hali hii inachelewesha pia uwezo wa kushika lugha; wengine hawasemi wengine wanaijifunza kwa matata. Kwa upande mwingine kuna maumbo ya hali hii ambako mtu ana uwezo mkubwa wa kukumbuka vitu, namba au hata kitabu kizima. Kuna wengine wenye akili juu ya kiwango cha kawaida lakini hata hivyo si rahisi kwa kuwaelewa watu wengine jinsi wanavyojisikia. Kuna pia hali kali ya autism ambako akili inabaki nyuma kabisa. --Kipala (majadiliano) 17:20, 19 Februari 2009 (UTC)

Bukoba Mjini

Kipala, salam. Sioni majina ya kata katika wilaya hii. Sasa sijui wewe mwenzangu umeoyaonaje? Naona miidadi ya watu tu, bila majina ya kata. Mmhh, mbona mauzauza (maajabu).--Mwanaharakati (Longa) 10:28, 21 Februari 2009 (UTC)

Wenzangu hawajambo. Nami pia sijambo! Nataka leo nifikishe 10,000 - halafu nitajulisha! Lakini ni leoleo.--Mwanaharakati (Longa) 11:08, 21 Februari 2009 (UTC)

10,000

Eti sijui nicheke ama niliye? Basi wacha tu ni furahi kuona kumi hizi! Ahadi yangu ya juu ilikuwa leo ni kufikisha elfu kumi - halafu niende zangu nyumbani. Basi naona muda umefika! Pia, niseme hongera kwa kuandika makala za miji ya Pemba na Unguja - kwani nayo ilisababisha kuifikisha elfu kumi hii kwa haraka zaidi! Hongera tele mzee wangu! Ni mimi wako kijana,--Mwanaharakati (Longa) 14:08, 21 Februari 2009 (UTC)

Mtumwa? Sijakupata bado. Lakini hii ni kazi yetu sote (ingawa wewe unajitolea kuwaandikia makala Waswahili), lakini bado ninasikia faraja kuubwa kupita kiasi kwa kuona Mzungu Mjerumani kama wewe uliyejitolea kuwaandikia makala Waswahili! Pia, ninahuzunika kwa kujiona mpweke kwenye mitandao hii ya Wikipedia. Si kitu. Hapa hakuna mtumwa, bali tunajituma! Ubarikiwe!--Mwanaharakati (Longa) 14:23, 21 Februari 2009 (UTC)
Ni kweli. Lakini hata nikiangalia Wikipedia za Kiafrika zoote (tukitoa ya Afrikaans), basi hamna kitu mbele ya Wikipedia kwa Kiswahili. Ninasikia raha (pia hata kujivunia) kwa kuwa na Wikipedia yetu pekee! Marafiki zangu wa nje, kwa mfano, wale wa Uturuki, Vietnam, Ufaransa, na Italia, wanaisifia ya kwamba, katika Wikipedia za Kiafrika, basi Wikipedia kwa Kiswahili ina makala nyingi sana ambazo kwenye Wikipedia zingine zipo (hasa za Ulaya)! Pia, hamna viandishi vifupi-vifupi kama Miwikipedia mingine ya Kiafrika! Basi hongera kwa makala zako juu ya uhandishi wa Kiswahili. Mungu akuzidishie maisha marefu kwako na kwa familia yako! Ahsante.--Mwanaharakati (Longa) 14:43, 21 Februari 2009 (UTC)
HONGERENI!!! Mmenifurahisha bila kikomo. Asanteni sana. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 19:25, 24 Februari 2009 (UTC)
Baada ya kimya kirefu, nawakuta mmefika mbali hivi! Pongezi zooote! Nitawaunga mkono hivi karibuni! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:19, 1 Machi 2009 (UTC)

Kukaribishwa

Asante kwa kunikaribisha hapo kwenye Wikipedia ya Kiswahili. Lloffiwr (majadiliano) 20:16, 23 Februari 2009 (UTC)

Tatizo

Mzee Kipala, nikusalimie kivipi? Shikamoo!!! Nimeelewa kuwa unanizidi kwa umri, watu humo wanakusalimia mzee, lakini ni mtu wa kuheshimu kwa kazi yako nyingi katika wikipedia ya Kiswahili. Nimefurahi kusikia ya kwamba kazi ya kuongeza makala yenye lugha yetu Kiswahili inaendelea vizuri, lakini watu wako wapi ambao wako tayari kuunga mkono kupanisha makala ya jamii ya mwili? Naomba misaada kwa watu wengi! Kama vile wewe, nimejifunza kiswahili kama mtu mzima, nimetoka nchi ya Sweden. Ya mwishomwisho, nina tatizo la kusajili akaunti yangu kwenye wikipedia. Umewahi kuwa na tatizo kama hilo? Ndimi Rehema.--80.78.216.4 22:28, 25 Februari 2009 (UTC)

Salaam Rehema au niseme "marasaba" yaani mambo ya mzee sitegemei naichukua kama utani wa kawaida upande wa rafiki yangu Muddy. Sasa kujiandikisha si vigumu (au wamebadilisha utaratibu?? Sidhani!) unaingia sw.wikipedia.org na kubofya "Ingia/ sajili akaunti" juu kwenye kona. Halafu kwenye dirisha linalofuata unachagua "Sajili akaunti". Wanataka uandike herufi zinazoonyeshwa ("To help protect against automated account creation, please enter the words that appear below in the box"). Halafu chini yake unaandika "Rehema" - sidhani imeshachukuliwa kwetu. Isipokuwa kama mtu ameshajiandikisha kwa jina hili - HAPANA naona akaunti ya Mtumiaji:Rehema iko. Je ni wewe? Au mwingine? Kama wewe: je umesahau password yako? Au tatizo ni nini?? Je unakosea herufi kubwa/dogo kwenye password? --Kipala (majadiliano) 22:44, 25 Februari 2009 (UTC)

Mimi ndiye Rehema huyo aliyeanza kutunga makala ya Figo, na hilo tatizo nimekuwa nalo kwa siku nyingi kadhaa. Baada ya kushindwa mara nyingi kuingia, nikajaribu ya mwisho kubonyeza ile kibonye "nitume nywila mpya kwa barua pepe" lakini hawakujibu, yaani wikipedia. Hivyo mimi sijui nifanyaje, ila kufungua akaunti mpya ambayo kulingana na maoni yangu isiyo lazima, maana nikiwa ninayo moja tayari.

Hakuna njia kukupa nywila mpya kama hujaandikisha email yako hapo mwanzoni. Au kama ulikosea anwani hii. Maana haya yote ni kazi ya tarakilishi tu. Ninaona njia mbili: A) Ninafuta akaunti ya mtumiaji:Rehema na wewe unajiandikisha upya kwa jina lilelile. (ILA TU: sina uhakika kabisa kama tutafaulu lakini nadhani angalau kwa makala ya kawaida inawezekana. Nikiona maelezo inawezekana tuache jina kjwa siku moja hadi imepita kwenye seva). B) Kuna njia ya usurpation ninafikiri mimi nina madaraka ya kuitekeleza lakini sina uhakika namna gani. subiri kidogo hadi jioni. --Kipala (majadiliano) 15:14, 26 Februari 2009 (UTC)

Ujumbe kwa Rehema: Ujiandikishe upya kwa jina lako. Nimehamisha akaunti yako ya kwanza, kwa hiyo hakuna akaunti tena kwa jina lako. Utumie nywila isiyo ngumu kwako na weka email yako. Hakuna atakayeweza kuona email yako (umeona jinsi ilivyo vigumu kwa password) kwa hiyo andikisha email maana ni njia rahisi kupata nywila kama ajali nyingine inatokea. Wasalaam --Kipala (majadiliano) 05:32, 27 Februari 2009 (UTC)

Asante nakushukuru! Baada ya kujiandikisha nitakutarifu tena hapa. //Nimewahi kujaribu kujiandikisha mara moja sasahivi, na Rehema bado ipo, nitajaribu tena wakati jioni na kesho, tuone!

Sidhani ya kwamba akaunti "User:Rehema" iko. Nimeijaribisha kwenye mashine mbili haiko tena. Nadhani ni kumbukumbu ya kompyuta yako tu. (kuna kumbukumbu ya "cache" kwa mashine za windowa inayokumbuka tovuti na ukirudia kuingia tovuti fulani inaharakisha mkasi kwa kuonyesha kwanza picha ya kumbukumbu badala ya kuchukua picha mpya kutoka nyavuni; ukipata tena ukurasa wa Rehema gonga "badilisha/hariri" utaona.--Kipala (majadiliano) 14:10, 27 Februari 2009 (UTC)
Kweli. Hamna akaunti ya jina la Mtumiaji:Rehema! Hata mimi nilioko Afrika naona kama hakuna akaunti hiyo. Basi ili aondoe cache - ni lazima afanye hivi: Bonyeza CTRL (usiachie) halafu bonyeza F5! Basi hapo itazunguka kisha itakuwa imefuta kumbukumbu za muda za internet (cache). Kazi njema.--Mwanaharakati (Longa) 14:29, 27 Februari 2009 (UTC)

Sielewi tarakilishi yangu inatatizo gani, maani ni mara ya tatu nimejaribu sasa na imeninyima kufungua akount mpya. Ujumbe ninaopata ni huu: "Kosa la kuingia Jina la mtumiaji uliloingiza tayari linatumika. Tafadhali chagua jina lingine". Tayari nimefuta kumbukumbu la kivinjari, sijui unamaanisha nifanye nini mwenzangu?

Nimeingia kwa jina mpya, sasa ni Amina badala ya Rehema. --Amina (majadiliano) 23:32, 28 Februari 2009 (UTC)

Nitaongeza zaidi juu yangu baadaye, ila tena ninawashukuru kwa msaada wenu wote.--Amina (majadiliano) 23:38, 28 Februari 2009 (UTC)

Ukipenda hivyo basi. Hata hivyo mtumiaji:Rehema iko tayari kuchukuliwa. Jaribu tu kujiandikisha. Kama cache yako bado inakupa picha ukurasa uko tayari basi bonyeza hariri nadhani utaambiwa juianzisha nisipokosei. Mara umeifanya naweza kuhamisha maandishi yako ya awali (iko kwa mtumiaji:Rehema-zamani). Baadaye naweza kufuta Rehema-zamani. Unaonaje??--Kipala (majadiliano) 12:57, 1 Machi 2009 (UTC)

Masomo ni mengi kwenye chuo wakati mwingine na nimechelewa kuandika hapa. Ningefurahi kama ungeweza kunisamehe na kuwa mwenye subira ukiwasiliana nami. Walakini nimepata nafasi kufikiri muda uliopita. Si mahitaji muhimu ya lazima maandishi yangu ya zamani yabaki kwenye akount ile ya Rehema. Nimewahi kuhamisha maandishi mengine lakini si yote. Mengine unaweza kufuta, tuanze majadiliano mapya kwenye ukarasa wangu! Karibuni tu! Tena, wote wawawili nawashukuru kwa misaada yenu.--Amina (majadiliano) 19:48, 5 Machi 2009 (UTC)

Basi sina neno nafurahi ya kwamba uko. Tumezoea ya kwamba wakinadada hubadilishabadilisha nywele yaani staili pamoja na rangi. Maadamu hapa tuko mahali pa maendeleo kabisa basi wakinadada wako huru kubadilisha jina vilevile. Nafurahi ya kwamba upo kwa jina lolote. --Kipala (majadiliano) 01:21, 6 Machi 2009 (UTC)

Umeshanipa kicheko kaka, maana ni kweli unayosema. Si miezi mingi iliopita nilipobadilisha rangi ya nyweli zangu. Kwa bahati mbaya nyweli zangu hazistahili kusukwa kama vile nyweli za kiafrika.--Amina (majadiliano) 15:20, 6 Machi 2009 (UTC)

Ushauri

Kipala, salam! Ninashida moja ya kutokuwa na maarifa mazuri ya kuweza kufupisha makala pale inapohitajika labda kufupisha. Mara nyingi ninanuiya kuandika makala fupi, lakini pia mara nyingi ninafeli na kujikuta ninaandika makala refu vilevile. Kwa sasa ningependa niandike makala fupifupi kama zile za Oliver (kuhusu watu waliopewa Tuzo za Nobel). Nami ningependa niandike kama zile, lakini aje? Ninatumai ya kwamba utanisaidia kwa hili! Ni mimi wako kijana,--Mwanaharakati (Longa) 06:41, 26 Februari 2009 (UTC)

Muddy, pole sana! Usikate tamaa nisipokosei ni wewe aliyeandika makala fupi kushinda sisi sote maana makala hizi za kata ni fupi sivyo. Lakini kama ni juu ya kichwa kingine mimi mara nyingi naangalia makala ya Kiingereza na kama ni kutafsiri tu wiki ya Kiingereza mara nyingi ina sehemu ya mwanzoni ambayo ni kama mhtasari wa makala yote. Kama ina maana inaweza kutosha kutafsiri sehemu hii lakini inaregemea na kichwa kama unaridhika na habari hizi. Unaonaje ?--Kipala (majadiliano) 15:32, 26 Februari 2009 (UTC)
Basi nitajaribu kufanya hivyo! Ingawa inaniwia vigumu kwani kila kitu kinakwenda na mazoea! Kingine, labda nifunge mkanda hadi kuwafikia wale Waafrikaans - wao wanamakala 11,600+ Hivyo ni kuongeza juhudi hadi kuwafikia! Ninaamini itakuwa. Kila la kheri na ahsante kwa ushauri!!!--Mwanaharakati (Longa) 16:28, 26 Februari 2009 (UTC)

Ping

Hi... i have answered you at [1] ++Lar: t/c 21:58, 26 Februari 2009 (UTC)

Kutokuwepo!

Kipala, salam. Leo (huenda ikawa hata kesho) sintokuwepo kwa kufuatia msiba wa pacha wangu (dada aliyefariki kwa uzazi baada ya upasuaji)! Ninasikitika kutokuwa nanyi kwa leo na kesho! Basi mbarikiwe na kila la kheri! Wenu kijana mtiifu,--Mwanaharakati (Longa) 06:24, 5 Machi 2009 (UTC)

Pole sana! NImeshtuka mno niliposoma habari hii. Naomba angalia barua pepe na ubarikiwe! --Kipala (majadiliano) 01:21, 6 Machi 2009 (UTC)

Pia mimi ninataka niwape poleni zangu kufiwa na ndugu yenu huko nyumbani.--Amina (majadiliano) 15:09, 6 Machi 2009 (UTC)


Porsche Museum

Hallo Kipala, da du scheinbar muttersprachlich deutsch sprichst, kann ich ja mit dir in meiner Muttersprache kommunizieren. Den Artikel Porsche Museum habe ich in einigen Sprachen bearbeitet und wollte ihn auch gerne in sw bereitstellen. Deshalb in englisch mit dem Hinweis "Translation" wie unten gezeigt.

Ich hätte jedoch mal eine grundsätzliche Frage: Ist es nicht erwünscht, dass man das Wissen der Welt auch in anderen Sprachen bereit stellt? Ich denke, gerade die schwachen Idiome wie sw sind besonders auf Unterstützung angewiesen. Ich wäre gerne bereit, hier mitzuarbeiten. Lass mich mal deine Meinung wissen. Danke.--RudolfSimon (majadiliano) 23:11, 8 Machi 2009 (UTC)

Schau doch bitte mal >>hier<<. Danke.--RudolfSimon (majadiliano)

Kiswahili

Thank you for the good word! I now have a good Kiswahili text book and am learning it from the beginning. My, isn't Kiswahili different from any other lanaguage I've encountered! I like a challenge! User:Jhendin (majadiliano) 00:14, 16 Machi 2009 (UTC)

Kata za Tanzania

Ninapenda kukushukuru kwa mshikamano wako juu ya ujenzi wa makala za mbegu za Tanzania. Nimemaliza ule Mkoa wa Tabora wote. Lakini bila msukumo wako, nahisi ningenyong'onyea! Shukrani kwa wazo lako la mbegu hizi, shukrani kwa ushauri na ujenzi wa vigezo vyote vya kata za wilaya ya Tanzania. Mungu akubariki, mzee wangu.--Mwanaharakati (Longa) 08:10, 16 Machi 2009 (UTC)

Tafsiri ya Agano la Kale

Ndugu, asante kwa kuanza kuweka viungo vya tafsiri hiyo katika makala husika. Ila sijaelewa kwa nini katika baadhi yake umeacha link ya Biblia Mwongozo, kumbe katika nyingine umeiondoa. Sikuiweka mimi, lakini najiuliza sababu yake nini? Amani kwa wote. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:44, 16 Machi 2009 (UTC)

Usamehe udhaifu wa mwili na roho. Nilikuta mara ya kwanza Biblia yote kwa Kiswahili iko mtandaoni (si Agano jipya tu!) nikafurahia nikaanza kuweka katika makala kadhaa. Nikakuta viungo vya "Biblia Mwongozo" na baada ya kuweka viungo kadhaa nimejaribisha kiungo kumbe hamna kitu tena. Nikafuta viungo kadhaa lakini sijarudi pale nilikuwepo awali. Nadhani viungo hivi viliingizwa na mtumiaji:CarlHinton aliyepakiza pia sehemu kubwa ya maandishi ya makala mbalimbali. Sijui kama unakumbuka tuliona alikuwa alinakili maandishi kutoka kijitabu fulani tukamwuliza kama alikuwa na kibali sasa sikumbuki jambo lilikwisha namna gani anyway hakupenda kujibu akapotea. Tovuti alipoelekeza viungo vyake imebadilishwa pia. Kwa hiyo tufute tu viungo hivi polepole kwa kushirikiana.--Kipala (majadiliano) 14:17, 16 Machi 2009 (UTC)
Ndugu, nakusamehe kwa moyo, tena sishangai, kwa sababu kazi yako ni kubwa sana! Kuhusu "Biblia Mwongozo", ni Baba Tabita aliyesema Carl Hinton aliingiza mada wakati hana hakimiliki. Lakini sijaamini sana. Mbona ndiye anayeshughulikia tovuti ya madhehebu yake? Tazama: "Swahili Language Christadelphian Booklets. Produced and Maintained by: Carl Hinton ... Click here to automatically translate Kiswahili words into English ...

www.cbm-tz.org/swahili/". Si kwamba napenda sana mitazamo yake, ila ni ndani ya mipaka ya sera ya Wikipedia. Au siyo? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:41, 20 Machi 2009 (UTC)

Nd Riccardo, nakubaliana nawe isipokuwa nimekuta ya kwamba viungo hivi vyote vya Carl Hinton havifanyi kazi tena kwa sababu inaonekana muundo kwenye tovuti yake umebadilishwa. Kwa hiyo kama nisipokosei ni bure tu. Au umekuta wewe njia ya kuweka kiungo hai kuelekea kwake? --Kipala (majadiliano) 16:19, 20 Machi 2009 (UTC)

Kigezo Mwigizaji 2

Kipala, salam. Eti kwako unaona tatizo la kigezo husika na jina hapo juu? Kwangu naona haitaki kufanya kazi - sasa sijui kama na wewe unaiona imevunjika kama jinsi ninavyoona mimi huku? Tazama makala Eric Balfour‎ uniambie kama kigezo kimejiunga! Nitashukuru kama utanifahamisha kuhusu hilo. Ni mimi wako kijana,--Mwanaharakati (Longa) 07:12, 21 Machi 2009 (UTC)

Nimehaha hadi nimegundua kilichokuwa kinatatiza! Eti kumbe kigezo hiki akitaki ukiwekee <br> katika uga zake. Na ndiyo maana imekataa kuunganisha sehemu za chini. Niliiwekea break katika sehemu ya kutaja kazi zake, yaani, mwimbaji<br> mwigizaji! Basi nishajua tatizo. Samahani kwa usumbufu! Kazi njema.--Mwanaharakati (Longa) 07:28, 21 Machi 2009 (UTC)