Mtumiaji:Kipala/Archive 5

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Biblia[hariri | hariri chanzo]

Ndugu, asante kwa maelekezo yako. Bila ya shaka napenda kushirikiana, ila sikujua mengi kati ya hayo uliyoniandikia. Nitakuwa macho zaidi, lakini mambo ya kujifunza ni mengi. Nikikosea, msahihishe nyinyi mliozoea zaidi. Kosa moja nililolitambua lakini sijui kusahihisha ni kwamba makala moja niliyoandika ina kichwa "Barua ya Kwanza kwa Watesalonike" badala ya "... Wathesalonike". Naomba urekebishe. Ile njia ya ku-redirect sijaielewa. Asante. Salaam!

Ndugu, pole kwa kazi nyingi unazoifanyia Wiki. Nasubiri bado uingize Deuterokanoni 7 katika lebo ya Agano la Kale. Pia nimeingiza ile ya Agano Jipya katika vitabu vyote vilivyokuwa havina, lakini kuna shida: imeandikwa Galata na Thesaloniki, tofauti na kurasa husika. Naomba uirekebishe mambo yawe sawa. Mimi siwezi. Hatimaye naomba tena uangalie usilinganishe "Biblia ya Kiebrania" na "Agano la Kale" kama ni kitu kimoja: kwa Wakristo walio wengi sivyo, kwa kuwa Agano la Kale lina vitabu 7 na sehemu nyingine ambazo hazimo katika Tanakh. Wasalamu --Riccardo Riccioni (majadiliano) 21:40, 16 Julai 2008 (UTC)

Namaanisha zile lebo zilizopangwa chini ya ukurasa "Agano la Kale" na ya vitabu vyake mbalimbali, zenye majina ya vitabu vyote yakiwa na viungo husika. Katika vitabu vya "Agano Jipya" viko pembeni.

Nimeelewa. Ilikuwa Template:Biblia_AK. Nimesahihisha. Halafu ilikuwa nini juu ya kulinganisha "Biblia ya Kiebrania" na "Agano la Kale"? --Kipala (majadiliano) 07:41, 17 Julai 2008 (UTC)

Tafuta katika dirisha la nje[hariri | hariri chanzo]

Kipala, salam. Nafurahia kuona na sisi Wikipedia kwa Kiswahili tunapatikana kwa asilimia 100 katika dirisha la tafuta la Google! Kila makala ya Wikipedia kwa Kiswahili, ukiitaka kuipata kiurahisi basi uende Gooogle. Yaani kama tumeingia nao mkataba wale jamaa. Ni kufurahia tu kwamba na sisi tutafahamika hivi karibuni. Pia zile ndoto zangu kuitaka Wikipedia watu wengi waijue natumai zinaendelea vizuri na wasanii wa Tanzania wao washaanza kupeana habari kuwa kuna mtandao ambao kila mtu anaweza kuhariri huru bila matata!! Basi hata mwaka huu ukisha naona tutakuwa tushafahamika vya kutosha. Basi ni hayo tu niliyokuwa nayo!! Likizo njema!!!--Mwanaharakati (majadiliano) 05:46, 1 Agosti 2008 (UTC)

Asante kwa salamu. Bado niko safari naangalia wakati mwingine tu kwa dakika. Sina nafasi ya kufanya kazi. Nadhani ni sawa google inasambaza wikipedia nadhani ni utaratibu wao wa ndani kuweka wikipedia juu. --Kipala (majadiliano) 02:46, 2 Agosti 2008 (UTC)

Sprichst du deutsch?--RudolfSimon (majadiliano) 17:54, 13 Agosti 2008 (UTC)

Stundenlang, wenns sein muss. Bin im Moment aber noch auf Reisen und nicht so oft am Netz. --Kipala (majadiliano) 01:22, 14 Agosti 2008 (UTC)

SUL request[hariri | hariri chanzo]

Dear bureaucrat. This is joseph from Turkish Wikipedia. I want to usurp the account named locally as "joseph" for SUL merge. Here is confirmation Thanks. (any message here please) --88.227.206.227 17:00, 17 Agosti 2008 (UTC)

Hi Kullanıcı, could you kindly explain your interest for publishing on sw-wiki? We have no policy for usurpation here and I do not see why I should cancel the -though presently inactive- account of a sw-speaker for someone who seems not to know the language. --Kipala (majadiliano) 22:09, 17 Agosti 2008 (UTC)
I asked usurpation, just and only, for SUL. If there's no policy for usurption, then it's all up to you. Thanks anyway. (joseph) --88.252.209.126 18:22, 19 Agosti 2008 (UTC)

Grüße aus der Nähe von Köln[hariri | hariri chanzo]

Hallo Kipala, die besten Anekdoten schreibt doch das Leben... von dem obigen Wortwechsel kannst Du doch glatt ein Screenshot machen und einrahmen!

Ich grüße dich aus der Nähe von Köln. Am Kiwusee ist meine Nabelschnur vergraben worden und als kleines Kind soll ich mal ganz gut Kiswahili gesprochen haben. Leider, ist von der Sprache in meinem "erwachsenen Kopp" nicht mehr viel zu finden, leider - nur schöne Erinnerungen an frühe Kindertage. Ich mache bei der Wikipedia in de, fr, pt und en mit - und wäre glücklich, wenn ich etwas beisteuern könnten zur sw Wikipedia! Auch ohne "account" ;-) Sei! --217.232.65.192 07:59, 26 Agosti 2008 (UTC)

Ja, es ist ein nettes Dokument. Ich habe leider keine Ahnung, was "SUL" bedeutet. Bürokrat wird man hier im virtuellen Afrika (leiblich sitze ich an der Elbe) wohl viel zu einfach. Seufz. (Wenn du Lust hast, etwas zu tun: Kannst du Karten, Grafiken etc??) --Kipala (majadiliano) 15:28, 26 Agosti 2008 (UTC)

Karibu tena![hariri | hariri chanzo]

Kipala, salaaam! Habari za likizo mzee wangu, natumai upo salama! Basi karibu tena katika Wiki yetu!! Mengineyo: Angalia vilivyojiri na uanze kuvipitia kama sahihi! Karibu sana.--Mwanaharakati (majadiliano) 06:01, 30 Agosti 2008 (UTC)

Asante kwa salamu! Niko. --Kipala (majadiliano) 16:20, 31 Agosti 2008 (UTC)

Kipoland[hariri | hariri chanzo]

Salam. Kipala, samahani. Unaweza kutoa mchango wa fikra zako katika mjadala huu? Maana naona vioja tu katika makala hiyo. --Mwanaharakati (majadiliano) 16:25, 1 Septemba 2008 (UTC)

Kijiji, kata, wilaya[hariri | hariri chanzo]

Salaam. Labda nijaribu:

1. Ward, ladle, administrative district yote ni moja, ambayo inamaana sawa ya KATA.

2. Kijiji, hapa napata VILLAGE pekee yenye kutaja KIJIJI.

3. District, hii ndiyo yenyewe inayotakiwa kuwa WILAYA.

Mengineyo: Mji na Kijiji viko tofauti kiasi. Mji, mpaka uteuliwe kuwa mji au jiji. Mara nyingi mpaka kuwe na mahitaji ya msingi yote ambayo si lazima kwenda mjini, hivyo yanapatikana hapo hapo katika kijiji, basi baadaye wanaubadilisha nakuiita mji! Hiyo kwa Bongo tu. Sijui huko kwingine. Haya, lako nishamaliza. Bado langu! Waweza kunipa machache kuhusu "FREEMASONRY" ?--Mwanaharakati (majadiliano) 06:17, 5 Septemba 2008 (UTC)

Oooh, sawa. Kijiji cha Umbweni kina KATA tatu. Inamaana kuwa KATA iko chini ya Kijiji! Kuhusu DIVISION: Baso sipati picha kamili katika kutaja myenendo ya sekta za serikali katika maeneo. Sipati picha zaidi ya kusema UGAWAJI! Nad ndiyomaana sijaiandika katika mjadala wa hapo juu. Sijui. Ila KATA iko chini ya KIJIJI. Hapo vipi?--Mwanaharakati (majadiliano) 05:53, 6 Septemba 2008 (UTC)

Hi Kipala ;)[hariri | hariri chanzo]

Hi! How are you? Could you please help me add a couple of sentences to the Kiswahili version of this interesting article?

Thanks so much! -Ivana Icana (majadiliano) 22:31, 6 Septemba 2008 (UTC)

Kilatini[hariri | hariri chanzo]

Ndugu, nimesikitika kwamba umekata habari nilizoandika kuhusu Lugha za Kirumi. Kilatini ni mama yake: ukitaka kumuelewa mtoto, ni muhimu kutaja na kufahamu wazazi! Si mpaka utumie kiungo... Naomba urekebishe mwenyewe. Kama hupendi kwamba nimetaja Kanisa Katoliki, futa hilo tu... --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:45, 21 Septemba 2008 (UTC)

Riccardo, labda afadhali ningetaja sababu zangu kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano kabla ya kusahihisha. Lakini hata hivyo tuko huru kama nimekosa basi tusahihishe upya. Sababu zangu ni hizi:
Kwa bahati mbaya sehemu za nyongeza zako katika makala hazikusaidia kuelewa "lugha za Kirumi" vema zaidi. Ni maelezo yanayohusu lugha ya kilatini. Kuna makala ya "Kilatini" na makala hii bado ni fupi inafaa kupanushwa. Sielewi unalilia nini kuhusu kanisa katoliki; ukiweza kuonyesha jinsi gani matumizi ya Kilatini kanisani yalikuwa muhimu kwa kutokea kwa lugha za Kirumi andika tu hapa; ila tu yale uliyotaja ni kuhusu maendeleo ya Kilatini chenyewe unaikuta katika makala yake (kanisa katoliki mara tatu nisipokosei hata kama ni makala mafupi tu).
Nimeona hasa nyongeza katika sentensi ya kwanza zilileta ugumu kuelewa kicha cha habari vema. Pamoja na hayo sioni ni kweli kusema Kilatini "kilikufa mwishoni mwa milenia ya kwanza"; ungesema kama Lugha ya kwanza afadhali lakini haina mahali katika sentensi ya kwanza ya makala hii; swali jinsi gani Kilatini kilikufa au hakikufa ni jambo la kujadiliwa hasa ukikumbuka nafasi yake kubwa kama lugha ya mawasiliano iliyoandikwa na pia kuzungumzwa katika Ulaya pamoja na ufufuo wake kama Kilatini Kipya wakati wa karne za 16-18. Ila tu maswali kama haya yana nafasi ndani ya makala yake si chini ya kichwa kingine.
Nahamisha mazungumzo haya kwenda ukurasa wa majadiliano ya makala yenyewe ni mahali pake. --Kipala (majadiliano) 11:00, 21 Septemba 2008 (UTC)

"Mchongo"[hariri | hariri chanzo]

Ninasema Kiswahili kidogo tu na nataka kuweza maana ya "Mchongo". Nikiangalia na kamusi, nikipata "notch" na "cut" tu lakini ninajua neno linamaana kingine pia. Nilitafuta ukurasa wa mtandao na "black supremacy" na "mchongo". Unajua zaidi? Asante kwa msada! Ozsvensk 14:24, 27 Septemba 2008 +1

Salam nyingi. Labda ningeingilia mada hii. "Mchongo" ni kama ulivyosema ("notch" na "cut"). Lakini kwa Kiswahili cha sasa, "Mchongo" ni "Kazi" au "Nafasi ya Kazi". Mfano: Nimesikia kuna "Mchongo" wa kazi pale katika kampuni yako unayofanyia kazi. Ni kweli?

Natumani utakuwa msaada tosha!! Basi karibu sana. Niite,--Mwanaharakati (Longa) 09:23, 10 Oktoba 2008 (UTC)

Asante sana, rafiki! Ni vigumu sana kusema Kiswahili sijapokuwa Bongo au Kenya. Pia, nitajaribu kuna Wikipedia ya Kiswhaili bas itakuwa rahisi zaidi kuongea na waswahili. Asante kwa msada! Ozsvensk 19:38, 12 Oktoba (GMT +1)

Countryside[hariri | hariri chanzo]

Kipala, salam. Ninashida ya kufahamu wakisema "countryside". Sielewi vyema ni nini hiyo countryside. Kwa mfano maelezo haya:

It is a popular destination for both domestic and foreign tourists, who use it as a base to explore the nearly countryside which is renowned for its beauty, especially the nearby Mount Ida (Kaz Dağı).

Ningependa kufahamu walielezea nini?--Mwanaharakati (Longa) 09:17, 10 Oktoba 2008 (UTC)

Countryside inaweza kumaanisha: mazingira ya mahali (yasiyo ya mjini); "going to the countryside" - kutembea eneo la mashambani, la vijijini; "beautiful countryside" eneo zuri, nchi nzuri (lakini si mji); katika sentensi ya juu: ningetafsiri tu "mazingira". --Kipala (majadiliano) 08:12, 20 Oktoba 2008 (UTC)
Ahsante kwa tafsiri kutoka Uswahilini! Nakutakia safari njema!--Mwanaharakati (Longa) 08:45, 20 Oktoba 2008 (UTC)

Pole![hariri | hariri chanzo]

Salam, Kipala. Pole na safari ya kutoka EAK/T! Nahisi umechoka, lakini naona umekuja kwa kasi kuubwa kabisa! Basi karibu na tuendelee kushirikiana!!! Nilikuwa na kukaribisha tu. Karibu tena!--Mwanaharakati (Longa) 08:33, 29 Oktoba 2008 (UTC)

Asante! Niko tu. Kazi tele hata hivyo najaribu. --78.51.136.81 10:02, 29 Oktoba 2008 (UTC)

Template:PD-self‎[hariri | hariri chanzo]

Kipala, salam! Haya, nimeoa umepakia picha ya image:Ziwa Tanganyika.PNG, huku ikiwa imeambatana sambamba kabisa na Hatilimiki ya "Leseni ya Umma", yaani PD-self kwa mujibu wa picha yenyewe jinsi inavyoonyesha kutoka katika chanzo. Basi nilikuwa nakuomba kama utapata kajimuda kadogo cha kutafsiri ile mistari nisipokosea "mitano", ambayo imeizungumzia template husika na kichwa cha habari hapo juu! Ni kweli imeandikwa Kiingereza rahisi, lakini ninahofu katika moyo juu ya zile terminology jinsi zilivyotaja ile template. Unafikiri unaweza kupata hako kajimuda ka dakika tano ka kutafsiri hiyo template?--09:04, 30 Oktoba 2008 (UTC)

Hi Kipala, my name is Ecemaml and I'm and administrator and bureaucrat in the Spanish Wikipedia (verify) and an administrator in Wikimedia Commons (verify). I'm trying to recover my user name in all the wikipedias it was maliciously squattered some time ago (you can see the SUL information here). I've been looking for a place for asking usurpation, but as long as I can read Swahili, and there is no interwiki to such a section, if existing, I've turner to directly ask it to an administrator (if there is such a section, please, don't hesitate to forward me to there).

You can see a proof of my identity in here. Could you please help me? Best regards --80.35.163.143 21:43, 18 Novemba 2008 (UTC)

Dear ecemaml, why don't you just register yourself? There is no user by your name (otherwise we have no usurpation policy) so it is probably faster just registering yourself instead of looking for an admin. --Kipala (majadiliano) 00:10, 19 Novemba 2008 (UTC)
Mzee wangu, salam. Naona utaki mchezo kabisa! Umetoa hukumu ya milele. Huyo jamaa nilimwona toka jana akiingiza huo ushenzi wake, sema nilimwacha kum-block kwani nilikuwa na mvutia muda tu. Lakini naona keshapewa kile ambacho ana stahili kuwa nacho! Basi tuendelee!--Mwanaharakati (Longa) 16:04, 19 Novemba 2008 (UTC)
Kipala, naomba nisaidie kutafsiri maneno haya ili niweze kuyaweka katika Jamii ya WAHUSIKA WA PRISON. Nimeshindwa Kuswahilisha!

Naomba msaada wako!--Mwanaharakati (Longa) 17:01, 19 Novemba 2008 (UTC)

Kimsingi itakuwa ni kitu kama "Wahusika wa filamu za tamthiliya mfululizo". Sasa: hizi filamu fupi za "soap" zinaitwaje? tamthiliya ya TV au filamu ya tamnthiliya? Utajua wewe. Halafu hizi "series" - ni filamu mfululizo? Lakini utajua wewe kuliko mimi, nadhani. --Kipala (majadiliano) 17:25, 19 Novemba 2008 (UTC)
Katika kutembea kwako Tanzania, usha wahi kuona watu wakicheza pata potea (karata tatu), ni mchezo mmoja wakuongopeana kupata ilhali hupati. Maanake hivi. Mimi nimeshindwa kutasfiri na ndiyomaana nimeomba msaada kwako mzee wangu we loh! Lakini haya, ngoja nijaribu tena!--Mwanaharakati (Longa) 17:29, 19 Novemba 2008 (UTC)

Help for Translation[hariri | hariri chanzo]

Hallo Kipala, kannst Du mir die Übersetzung für: Flammenfärbung durch XYZ sagen?!? Danke und Gruß HBR (majadiliano) 22:47, 28 Novemba 2008 (UTC)

Zeige bitte mal 2 Stellen, wo das vorkommen sollte. Das muss eine Umschreibung sein, als tt gibt es das vielleicht nicht. --Kipala (majadiliano) 22:57, 28 Novemba 2008 (UTC)
Als Bildunterschrift in der Gallery von: Stronti oder bei Natiri HBR (majadiliano) 23:41, 28 Novemba 2008 (UTC)
Schau mal bei Natiri - prima, wenn du noch ein paar Flammprobenbilder einbauen magst! --Kipala (majadiliano) 14:39, 29 Novemba 2008 (UTC)

Renaissance[hariri | hariri chanzo]

Kipala, salam! Katika pitapita zangu kwa kuangalia makala za wasanii, nimegundua katika makala ya Raphael kuwa kuna maneno yameandikwa: alikuwa msanii wa zama za mwamko. Hizi zama za mwako ndiyo hii "Renaissance?" Nina shida ya kujua hii zama za mwamko kwa Kiingereza waliitaje? Samahani sana!--Mwanaharakati (Longa) 15:48, 1 Desemba 2008 (UTC)

Ni kweli, nimeongeza maneno kule kwa mabano na kuweka kiungo. Je unaonaje neno linaleweka? Kamusi zina majaribio tofautitofauti lakini nilichoona hadi sasa wanatumia "mwamko". --Kipala (majadiliano) 07:45, 2 Desemba 2008 (UTC)
Mzee wangu, salam. Ni kweli. Neno linaleta maana nzuri kabisa. Na pia nimeshukuru kujua ya kwamba kuna makala ya Middle Age, yaani ile inge nighalimu. Nilikuwa na mpango kuandikia makala yake. Lakini naona ipo, basi sasa hivi nitakuwa nauliza! Hata hivyo niliangalia katika makala za Simple sijaiona. Nahisi MABOT yameshaanza kuwa na mdororo! Basi tuendelee kushauriana katika makala hizi za kale! Ubarikiwe.--Mwanaharakati (Longa) 09:02, 2 Desemba 2008 (UTC)

Miji[hariri | hariri chanzo]

Kipala, salam. Ni kweli usemavyo na hata mimi nilifikiria kufanya hivyo tangu awali, sema nilikuwa navutia mda Kingine, mara nyingi hufanya kitu kwa mzuka vile unavyonipeleka niwe, lakini wazo lako ni la msingi sana Ahsante kwa ushauri wako--Mwanaharakati (Longa) 06:09, 6 Desemba 2008 (UTC)

Nina swali kidogo. Nataka kujua matumizi mazuri kabisa ya neno "However" Au nipe tasfri hii:
  • However, if they have, this permission likely does not fall under a free license.

Nitakuwa mwenye kushukuru endapo utanisaidia kutafsiri hilo likiwasambamba kabisa na maelezo yake ili kurahisisha kazi Wasalaam!--Mwanaharakati (Longa) 10:08, 6 Desemba 2008 (UTC)

However mara nyingi ni kama "lakini"; hapa maana yake ni "hata hivyo". "Hata hivyo kama wanacho kibali hiki uwezekano ni mkubwa ya kwamba hakilingani na ..." --Kipala (majadiliano) 10:35, 6 Desemba 2008 (UTC)
Ahsante sana Mzee wangu--Mwanaharakati (Longa) 10:52, 6 Desemba 2008 (UTC)

Kipala, salam! Ninashida kidogo katika kutafsiri "I Wish It Could Happen Again". Naomba nisaidie hapo mzee wangu--Mwanaharakati (Longa) 12:58, 10 Desemba 2008 (UTC)

Ni ombi la mtu anayependa jambo lirudie au litokee tena. Ila anajua haiwezekani kwa hiyo hasemi "that it happens again" lakini "it could happen again" - kitu kama "ningependa iweze kutokea tena"; au njia nyingine inayoonyesha anataka lakini anajua haiwezekani. --Kipala (majadiliano) 13:02, 10 Desemba 2008 (UTC)
Kumbe kweli bila wazee mambo hayaendi!!! Nashukuru sana kwa msaada wako--Mwanaharakati (Longa) 13:29, 10 Desemba 2008 (UTC)

Tafsri[hariri | hariri chanzo]

Kipala, salam. Unaweze kutupa macho katika ukurasa wa kona ya majadiliano ya wikipedia? Kuna swali nimeliacha pale ili watu watoe mawazo yao--Mwanaharakati (Longa) 14:28, 15 Desemba 2008 (UTC)