Mtumiaji:Kipala/Archive 1

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Archive Hii ni ukurasa wa Hifadhi ya Majadiliano ya Awali. Usihariri ukurasa huu usiongeze wala kupunguza kitu.
Ukitaka kujadiliana upya mambo yaliyomo humo nenda kwa ukurasa wa majadiliano ya sasa.
Kipala, asante sana kwa kunikaribisha. Kuhusu majina ya nchi, kuna orodha nzuri inayopatikana kwenye Kamusi Hai. Orodha hii inafuata orodha tatu nyingine: zile za BAKITA, TUKI, na Redio Tanzania Dar es Salaam. Vikundi hivi vitatu vilisanifisha (au viliswahilisha, ukipendelea) majina ya nchi zote za dunia. Kama ulivyosema, mara nyingi hakuna makubaliano baina ya vyanzo mbalimbali, na orodha hiyo ya Kamusi Hai inaonyesha mitafaruku. Lakini kwa jumla orodha ya Kamusi Hai inaonyesha majina yaliyopendekezwa na wataalamu wa vyuo na waandishi wa habari. Je, tufuate mapendekezo haya, au tuhimize istilahi nyingine ya Kiwikipedia? Nafikiri ni afadhali tufuate njia moja na wao waliopewa cheti kusanifisha lugha rasmi, lakini naomba shauri lako.
Orodha ya TUKI ilichapishwa katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Toleo la Pili, mwaka 2004, kurasa 473-477. Orodha hii ilifuata mapendekezo rasmi ya orodha ya BAKITA kutoka mwaka 2001, lakini ilibadili maneno mbalimbali (Ekwado badala ya Ikwado, kwa mfano). Baada ya hapo, Redio Tanzania Dar es Salaam ilipendekeza mabadiliko mengine mwaka 2005, kufuatana na matumizi yao. Mapendekezo yote yanaonekana katika orodha ya majina ya nchi iliyoandaliwa na Kamusi Hai ya Kiswahili kwenye Mtandao. Malangali 18:04, 23 Juni 2006 (UTC)



Kipala, unakaribishwa kujiunga kwenye kikundi cha mazungumzo kuhusu mawikipedia ya lugha mbalimbali za Kiafrika. Naomba utembelee http://groups.yahoo.com/group/afrophonewikis/ kujiandiksha. Asante, Malangali 19:21, 16 Agosti 2006 (UTC)

Maswali magumu Kipala. Unaonaje nikiweka maswali haya pale kwenye kamusi hai mtandaoni? Binafsi ninapendelea "gamba" zaidi ya "ganda." Na "kiini" zaidi ya "masoka". Sioni ubaya kwenye kuazima neno na hivyo kutumia "manto." Unaonaje tukiuliza? --Ndesanjo

Ni vizuri ukiuliza. Labda itavuta wengine katika mradi huu. "Koti" unaonaje? Vipi wazo la Templeti na maneno yake? --Kipala 21:51, 2 Septemba 2006 (UTC)

Kipala, nimejaribu kuweka jedwali kuhusu BBC lakini limekataa. Msaada? (ndesanjo)

Samahani sijaelewa swali. Naona umehariri makala ya BBC. Tatizo ni nini? (kipala)

Nimeona sehemu mbalimbali (nje ya Wikipedia) zikitumia Jamhuri ya Kijerumani kama ilivyo kwenye Wikipedia. Kwanini isiwe Jamhuri ya Ujerumani? --Ndesanjo

Ni swali la utafsiri. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani iliitwa "Deutsche Demokratische Republik" - ilitumia neno "deutsch" ambalo ni "kijerumani" likitaja tabia au pia lugha. Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani (Bundesrepublik Deutschland) linatumia neno "Deutschland" linalotaja nchi yenyewe. Kipala

Hello Kipala. Now that you are back, I would like to draw your attention to something which I find difficult to explain in Swahili. Have you noticed that since a while the lines that separate the sections of the articles are visible inside the taxoboxes? This is not the case in other Wikipedias. Can this be fixed? ChriKo 21:42, 13 Septemba 2006 (UTC)

Saw the same. No idea. Pass it to admins --Kipala 22:30, 13 Septemba 2006 (UTC)


Naam kipala...

Hii ni kuonyesha ni jinsi gani nimefurahishawa na jinsi ulivyo hariri na kupangilia makala kuhusu Ubuddha. Kwa kweli imependeza!! Naomba uiangalie nyingine iliyopo kwenye majadiliano kuhusu Ukristo ningependa kuifupisha lakini kuna baadhi ya vielementi naona bado ni muhimu ukizingatia bado ninaiendeleza ili baadae ichujike. Hongera umechuje vizuri ile ya Ubuddha... Hii ya Ukristo naomba tusaidiane nayo ije kupendeza.

Upendo,

Moses


Kipala,

nashukuru kwa shauri lako... Ile makala ya "Ukristo" nadhani mbele nitaivunja kuwa Viungo tofauti vingi. Kwa mfano: Musa, Majia, majusi (Magic, Astrology), ilimu (esoteric), alikimu(alchemy), ginosia (gnosis), Agano la kale, Agano Jipya, Historia ya Kanisa, Nembo za kiilimu (esoteric seals and symbols), mafundisho, Kanisa zamani na sasa. Hivyo ninashauku ya makala nyingi. Labda na wewe umegundua sijamaliza; kwa kuwa nahitaji kwanza na makala ya mjadala kwani maneno mengi nimebuni mwenyewe na nitazidi kuyaleta. Kwa kweli inahitaji kutulia na wala sina haraka. Nikimaliza vipande vya sasa, nitasonga kwenye mambo ya sayansi. Naomba uendelee kufuatilia na kama utaanza kuona maana, ruhusa kuvunja makala na kutengeneza makala tofauti zenye kuingiliana.

Ahsante

Hujambo Kipala, habari za siku nyingi? ninanfurahi kupata ushauri kutoka kwako, tayari nimeufanyia kazi, ahsnte kwa kunikumbusha. --Joel Niganile 16:43, 22 Julai 2007 (UTC)


Kipala, kuhusu tarakishi au tarakilishi. Je matumizi ya tarakishi yapo wapi na wapi? Mradi wa Kuswahilisha Programu Huria (ule wa Kilinux), magazeti ya Kiswahili tarakilishi inatumiwa. Lakini inawezekana sio sahihi. Je hii umepata wapi? Tushauriane. --Ndesanjo 14 Agosti 2007

Ndesanjo, samahani nimechelewa kuona swali lako lakini sasa kuhusu tarakishi / tarakilishi. Nadhani kuna maneno haya yote mawili. Mimi mwenyewe natumia zaidi "kompyuta".
Tuone:
Ukiona ni muhimu basi usogeze makala ukisahihisha maneno. Sina neno. Kwa sasa nimeongeza redirects na kuongeza "tarakilishi" kama jina la pili ndani ya makala. --Kipala 15:02, 27 Agosti 2007 (UTC)

Muddyb Blast

Ahsante Ndugu Kipala zaidi ya Vipala kwa kuni karibisha kwenye Wikipedia na mi pia ni Miongoni mwa wana harakati kuiwezesha Wikipedia ya Kiswahili kuwa juu zaidi. hivyo Tushirikiane. Muddyb Blast Producer E-Mail- Muddybtz@yahoo.com, Mikito45@yahoo.com, Maendeleotz@yahoo.com


Muddyb Blast

Swadaktaa. Mimi nipo tayari kwa hilo kwani huku niliko ni Rahsi kuwapata hao wasanii na kuzungumza nao ni kiasi cha kuamua jumapli moja kuwatafuta wapi nitawapata na kuanza kufanya nao Mahojiano. Ndugu nina maswali kdahaa kuhusiana na wewe binafsi pia ki Wikipedia Kwanza binasi

  • 1 Wewe ni Mmoja wa Viongozi wa Wikipedia?
  • 2 Vipi makala ninazo andika zitapatikana kwenye Search Engene?
  • 3 Upo Uwezekano kupakia zaidi ya File moja la picha Kwenye Wikipdeia?.

Ni hayo sina mwengi zaidi mkubwa ila kuhusu Wasaanii umefanikiwa nitawatafuta na kufanya nao Mahojiano unaweza kutembela moja kati ya makala ambazo mimi nimeanadaa ni Professor Jay Inspector Haroun na Nyingine nyingi tu. Tupo pamoja wala usihofu kuhusu kuindeleza Wikipedia

Ndugu MuddyB, asante kwa jibu la haraka. Nashukuru na kufurahia ya kwamba utasaidia koboresha mradi wetu. Kuhusu maswali yako:
  • 1 Mimi si kiongozi wala hatuna viongozi. Lakini kuna vyeo vya huduma kama vile "wakabidhi" (http://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Wakabidhi) wanaoitwa "sysop" penginepo na mimi ni mmoja wao. Kwa jumla tuko wachache sana wanaoshiriki mara kwa mara; katika miaka miwili iliyopita tulikuwa watu wasiozidi kumi waliochangia mara kwa mara na wawili, watatu walichangia makala mengi. Kwa jumla hadi sasa ni zaidi Waafrika walio nje na Wazungu waliokaa TZ au EAK. Kwa hiyo twafurahia sana kila safari mwenyeji wa palepale kupiga hodi. Kumbe sasa ni kundi!
  • 2 Makala unazoandika zapatikana kwenye injini tafuti. Kwanza ndani ya injini ya sw-wiki (hii inaweza kuchukua siku kadhaa). Pia nikiweka jina lako kwenye google nakupata mara moja, vilevile "nako 2 nako".
  • 3 Kuhusu picha: uko huru kupaka picha nyingi. Isipokuwa sharti ueleze ya kwamba una haki za picha hizi. Hadi sasa -kwa sababu idadi yetu ilikuwa ndogo- hatujakuwa na matatizo kuhusu puicha lakini najua ya kwamba katika wiki za lugha mbalimbali picha ni tatizo kubwa kwa sababu za sheria za hakimiliki. Yeyote anayeweka picha anatakiwa kueleza ya kamba yeye ndiye mwenye hakimiliki ya picha hiyo na ya kwamba anapaka picha hii kwenye wikipedia kwa matumizi ya umma bila masharti yoyote. Hapa naona tungepaswa kuchungulia picha zilizopakwa juzi na wenzetu lakini hatujaanza bado sijui nani atafanya.
Basi ukiwaona wenzako wasalimie ningependa sana kuwa nanyi huko Dar lakini kwa sasa sina ila kustahimili hali inayoitwa "majira ya joto" hapa Ujerumani niliko. --Kipala 12:53, 28 Agosti 2007 (UTC)

Muddyb Blast

Naam mkubwa nimekupta vilivyo na nimejaribu kutafuta zile baadhi ya makala nimeziona karibuni zote kwenye Google lakini kweny Yahoo bado sijafahamu kwanini lakini hamna neno zita appear soon kinachotakiwa ni Subila kila kitu kitakuwa pia unaweza kuhariri zile makala kwa uoande lugha huenda nikawa nimeandika lugha ambayo watu wengine wanaweza wasizielewe hivyo Tushirikiane. Mimi binafsi nime amua kuwa Mwana Wikipedia sasa basi hizi fikra zangu sitaki zigonge mwamba kwaivyo Mr Kipala along with Mr Ndesanjo, Oliver, nk. Msiinitupe mkono tuwe kwa kila atua, mimi nitabaki kwenye sekta ya Muziki na Filamu nitawafuatilia kwa undani ili hizi makala za wikipedia ziwe za uhakika zaidi na kuaminika hivyo naomba msaada wako mzee kipala katika kuendleza hizi makala zangu na kila makala ambayo mimi nime andika nitazirekebisha na kuhakikisha kuwa zime kuwa za kweli na bora zaidi. kila la kheri mzee kipala wa ujerumani pole na joto Muddyb Blast Producer

Archive Hii ni ukurasa wa Hifadhi ya Majadiliano ya Awali. Usihariri ukurasa huu usiongeze wala kupunguza kitu.
Ukitaka kujadiliana upya mambo yaliyomo humo nenda kwa ukurasa wa majadiliano ya sasa.