Mtumiaji:Kemyjr
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Lugha | ||||
|---|---|---|---|---|
|
Mimi naitwa Lina Joseph Rujweka,ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar-es-salaam, ninayesoma shahada ya sayansi ya tarakilishi, mwaka wa tatu. Jinsia yangu ni ya kike. Ni mtoto wa tatu kuzaliwa katika familia yenye watoto watano kati yao wakiwemo wasichana watatu na wavulana wawili. Kabila langu ni Mnyambo, mwenyeji wa mkoa wa Kagera, wilaya ya Karagwe,katika kijiji cha Kibona. Mimi ninazungumza lugha ya kiswahili na kiingereza.
Nimefurahi sana kuchangia kamusi elezo huru kupitia ushiriki wangu katika shindano hili la Wikipedia ya Kiswahili la 2009. Lengo hasa ikiwa ni kukuza lugha ya kiswahili. Ni matumaini yangu waafrika wengi watanufaika na kamusi elezo huru katika nyanja mbalimbali kama vile utafiti.