Mtumiaji:Kandyzo/Trip lee

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Trip Lee
Trip Lee

Historia[hariri | hariri chanzo]

William Lee Barefield III, anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii, "Trip Lee", ni mwimbaji wa nyimbo za Kikristo ambaye amejijengea jina akiimba akiwa pekee yake na pia akiwa mwanachama mwanzilishi wa kikundi cha 116 Clique. Hapo mwanzoni aliishi katika jiji la Dallas, Texas, [1] lakini yeye sasa anaishi katika mji wa Philadelphia, Pennsylvania. Trip Lee ana mkataba na Reach Records ,walio na makao yao makuu Marekani, na huko ndiko anakorekodi nyimbo zake. Yeye alipata sifa baada ya kuonekana kwenye tovuti ya Reach Records ,akiwa umri wa miaka 16, akiwa ameandika makala machache juu ya dini ya Kikristo na kuonyesha maarifa yaliyozidi kijana wa umri wake. Albamu yake ya kwanza, If They Only Knew, ilitolewa mwaka wa 2006. Albamu yake ya pili, 20/20, ilitolewa tarehe 20 Mei, 2008 na ilinunuliwa sana kwenye iTunes Music Store[1]. [2]


Taawasifu[hariri | hariri chanzo]

Barefield alizaliwa na kulelewa katika jiji la Dallas, Texas. Baada ya masomo ya shule ya upili, yeye akahamia ndani ya mji wa Philadelphia ambapo yeye huhudhuria Epiphany Fellowship (wakiongozwa na Eric Mason) huku akisoma katika Chuo Kikuu cha Kibilblia cha Philadelphia. Yeye alikuwa msanii wa tatu aliyetoa albamu yake ya kwanza na Reach Records. [5] Ili kupigia debe albamu hiyo ya kwanza na albamu ya 13 Letters,, Barefield na wenzake katika kikundi cha 116 Clique walisafiri kote Marekani wakiimba nyimbo zilizokuwa kwenye albamu hizo. Trip Lee na wenzake kama Tedashii, walipata sifa sana kwa kumsifu Yesu Kristo katika mtindo wao wa kuimba. Mwaka uliofuata,alichaguliwa kama mshindani kwa tuzo la GMA Dove Award kwa mchango wake katika wimbo wa Lecrae, Jesus Muzik.

Katika mwaka wa 2008, albamu yake ya pili,20/20, ilitolewa na ikapewa sifa na mashabiki kote kuliko albamu zake za hapo awali.Albamu hiyo ilinunuliwa zaidi ya zile zingine zote. Albamu hiyo ,20/20, ilikuwa na mafanikio hadi likatokea kwenye chati ya Billboard Top 200 ,inayoangazia albamu 200 bora zaidi duniani, na pia kwenye chati ya Top Christian Albums,inayoangazia albamu bora zaidi zenye nyimbo za Kikristo. Katika mwaka wa 2008, alienda ziara iliyoitwa Unashamed na wasanii wenzake Lecrae, Tedashii na Sho Baraka [9] huku wakitangaza injili.

Albamu ya Trip Lee ya Pili: 20/20
Albamu ya Trip Lee ya Pili: 20/20


Hapo tarehe 23 Mei 2009,Barefield alimwoa Jessica Ruccio mle Texas,siku chache tu baada ya baba yake kufa.


Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Albamu

   * If They Only Knew (2006)
   * 20/20 (2008)

Albamu akiwa na 116 Clique

   * The Compilation Album (2005)
   * The Compilation Album:Chopped & Screwed (2006)
   * 13 Letters (2007)
   * Amped (2007)

Nyimbo alizoshirikishwa

   * "What We Did" (Trip Lee akimshirikisha Tedashii )
   * "In Ya Hood Cypha" (Tedashii akiwashirikisha Thi'sl, Json, Sho, Lecrae & Trip Lee)
   * "Jesus Muzik" (Lecrae akimshirikisha Trip Lee)
   * "Holla At Me" (Everyday Process akimshirikisha Trip Lee)
   * "The Last Cypha" (The Cross Movement akiwashirikisha R-Swift, Everyday Process, Da 'Truth, Flame & Trip Lee)
   * "Price Tag" (Da 'Truth akimshirikisha Trip Lee)
   * "Slow It Down" (Sho Baraka akimshirikisha Trip Lee)
   * "What It Do" (Json akiwashirikisha Titus & Trip Lee)
   * "Checkin For My God" (The Ambassador akiwashirikisha Trip Lee & Lecrae)
   * "Fall Back" (Lecraeakimshirikisha Trip Lee)
   * "I Been Redeemed" (FLAME akimshirikisha Trip Lee)
   * "Ridaz" (JR akiwashirikisha Trip Lee & Iz-Real)
   * "I'm A Believer" (Tedashii akiwashirikisha Tedashii Trip Lee & Soyé)
   * "Transformers" (Tedashii akiwashirikisha Lecrae & Trip Lee)
   * "Trumpet Blow" (Da Truth akimshirikisha Trip Lee)
   * "Where Ya At" J(Legacy Conference) *

Tazama pia

   * 116 Clique[2]
   * Reach Records[3]



Viunganishi vya nje[hariri | hariri chanzo]

   * Reach Records[4]
   * [11]

Reach Records[5]

Wasanii wa nyimbo za Kikristo[6]

Wanamuziki kutoka Philadelphia, Pennsylvania[7]

[1] ^ Holy Hip Hop Database - Trip Lee [www.hhhdb.com/] [2] ^ "Trip Lee 20/20 afanikiwa katika Duka La Muziki la iTunes"[8] [3] ^ Maoni ya watu kuhusu albamu 20/20[9] [4] ^ Tawasifu katika Billboard.com[10] [6] ^ Daily Toreador 4/7/06[11] [7] ^ - Trip Lee - 20/20[12] [9] ^ Unashamed Tour[13] [10]^ Holy Hip Hop [www.holyhiphop.com/]