Mtume Mathia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mtume Mathiya)
Rukia: urambazaji, tafuta
Mt. Mathia alivyochorwa na Simone Martini.
Mitume wa Yesu

Mtume Mathia (kwa Kigiriki Matthias kutokana na Mattathias, kwa Kiebrania Mattithiah, maana yake "Zawadi ya Mungu") kadiri ya Matendo ya Mitume 1:21-22 alikuwa mfuasi wa Yesu Kristo tangu alipobatizwa na Yohane Mbatizaji hadi alipopaa mbinguni.

Kabla ya Pentekoste Mtume Petro alipendekeza mmoja kati ya wafuasi wa kwanza wa Yesu ashike nafasi ya marehemu mtume Yuda Iskarioti, na bahati ilimuangukia Mathia.

Ingawa Biblia haina habari zaidi juu yake, anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 14 Mei (Kanisa Katoliki na Anglikana), tarehe 9 Agosti (Waorthodoksi wa Mashariki) na tarehe 24 Februari (Walutheri na wengineo).

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: