Mtume Mathia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtume Mathia kadiri ya Matendo ya Mitume 1:21-22 alikuwa mfuasi wa Yesu Kristo tangu alipobatizwa na Yohane Mbatizaji hadi alipopaa mbinguni.
Kabla ya Pentekoste Mtume Petro alipendekeza mmoja kati ya wafuasi wa kwanza wa Yesu ashike nafasi ya marehemu mtume Yuda Iskarioti, na bahati ilimuangukia Mathia.
| Mitume wa Yesu |
|---|
|
Kwa Kigiriki jina Matthias linatokana na Mattathias, kwa Kiebrania Mattithiah, maana yake "Zawadi ya Mungu".
