Mtopetope

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtopetope
(Annona squamosa)
Mtopetope
Mtopetope
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Magnoliids (Mimea ambayo maua yao yana mizingo ya tepali tatu na chavua yenye kitundu kimoja)
Oda: Magnoliales (Mimea kama mparachichi)
Familia: Annonaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mkonokono)
Jenasi: Annona
Spishi: A. squamosa
L.

Mtopetope ni mti mdogo wa familia Annonaceae. Matunda yake yanayolika huitwa matopetope. Spishi hii huitwa mtomoko pia, lakini tafadhali jina hili litengee kwa Annona cherimola. Mti huu una maua madogo njanokijani yenye petali nene. Matunda yana umbo wa donge na rangi ya majani hadi manjano yakiwa yaliyoiva. Nyama ni nyeupe yenye ladha tamu. Mbegu nyeusi ni kubwa kiasi.

Picha[hariri | hariri chanzo]