Mto Songwe (Mbeya)

Majiranukta: 9°43′07″S 33°56′18″E / 9.7186°S 33.9383°E / -9.7186; 33.9383
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mto Songwe)
Mto Songwe (juu kushoto).

Mto Songwe ni jina la mito miwili ya Tanzania Kusini Magharibi: mmoja uko katika mkoa wa Mbeya (Songwe ya Kusini), mwingine katika mkoa wa Songwe (Songwe ya Kaskazini).

Songwe ya Kusini ina chanzo chake katika milima ya Umalila karibu na Santilya ikielekea kusini. Baada ya kupita Itumba (Ileje) mto ni mpaka kati ya Tanzania na Malawi hadi Ziwa Nyasa. Maji yake yanaishia katika bahari Hindi kupitia ziwa hilo na mto Zambezi.

Tabia yake ya kubadilisha-badilisha mwendo wake imesababisha matatizo kati ya nchi jirani kwa sababu mashamba ya watu yamepatikana mara upande mmoja mara upande mwingine wa mpaka wa kimataifa.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

9°43′07″S 33°56′18″E / 9.7186°S 33.9383°E / -9.7186; 33.9383