Msawazo
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msawazo ni hali ya usawa (ulinganisho, urari) kati ya athira au kani zinazopigana. Kama athira zinasawazika kuna hali ya msawazo.
Mifano [hariri]
Katika umakanika (fizikia) msawazo ni hali ambako kani tofauti zinasawazika kwa mfano kwenye wenzo kama zao la kani na urefu wa mkono kani ni sawa na zao la mzigo na urefu wa mkono mzigo.
Katika uchumi kuna msawazo kama kiasi cha bidhaa sokoni kinalingana na mahitaji ya wateja.
Samaki zinaweza kufika katika hali ya msawazo kwa kushika kiasi cha hewa ndani ya miili yao kinachosababisha kiwango cha ueleaji sawa na nguvu ya graviti inayowavuta chini. Kimsingi nyambizi (sabmarini) inatumia mtindo huohuo kwa njia ya hewa katika tangi yake.