Mr. & Mrs. Smith

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mr. & Mrs. Smith
Mr and mrs smith poster.jpg
Imeongozwa na Doug Liman
Imetayarishwa na Akiva Goldsman
Arnon Milchan
Imetungwa na Simon Kinberg
Nyota Brad Pitt,
Angelina Jolie,
Vince Vaughn
Kerry Washington
Adam Brody
Muziki na John Powell
Imehaririwa na Michael Tronick
Imesambazwa na 20th Century Fox
Imetolewa tar. Juni 10, 2005 (2005-06-10)
Ina muda wa dk. Theatrical cut
120 minutes
Unrated cut
123 minutes
Nchi Marekani
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu $110 million
Mapato yote ya filamu $478,336,279

Mr. & Mrs. Smith ni filamu ya 2005 yenye kupigana na kuchekesha iliyotayarishwa na Doug Liman na kuandikwa na Simon Kinberg. Muziki wake ulitungwa na John Powell. Wahusika wa filamu hii ni Angelina Jolie na Brad Pitt.

Yaliyomo

[hariri] Hadithi

Filamu hii inaanza pindi John (Brad Pitt) na Jane Smith (Angelina Jolie) wanajibu maswali yanayohusu ndoa yao. Maharusi hawa waneoana kwa muda wa "miaka tano au sita", lakini ndoa yao inapata pandashuka nyingi hadi wawili hawa hawajui ni lini mwisho walifanya kitendo cha ndoa. Wanaeleza jinsi walivyokutana kwa mara ya kwanza mjini Bogotá, Colombia baada ya kufukuzwa na askari. Walipendana baada ya hapo na kuoana.

Wote hawa ni wauaji wanaofanya kazi makampuni tofauti, na wote wanaficha siri hii. Jane na John wanatumwa kumuuwa Benjamin Danz. Baada ya kugunduana, wapenzi hawa wanapigana na kutaka kuuana. Baada ya kupigana kwa muda mrefu, Jane anamshikia bunduki mumewe lakini anashindwa kkupiga risasi kwa ajili ya mahaba aliyonayo. Hivyo basi, wote wanakumbatiana na kuanza upya mapenzi yao.

Kwa bahati mbaya, rafiki yake John aitwaye Addie anatumwa kuwaua John na Jane kisha atapewa $400,000. Hivyo basi, familia ya Smiths inaamua kupigana kwa pamoja ili kuokoa ndoa yao. Mwishowe, Jane na John wanashirikiana vizuri kuwaua kundi la wanajeshi waliotumwa kuwamaliza.

Filamu hii inamalizika pindi wawili hawa wanaenda kwa mkutano kuhusu ndoa yao, ambapo wanasema jinsi walivyo na raha wakiwa pamoja.

[hariri] Wahusika

  • Brad Pitt - John Smith
  • Angelina Jolie - Jane Smith
  • Vince Vaughn- Eddie
  • Kerry Washington - Jasmine
  • Adam Brody - Benjamin "The Tank" Danz
  • Keith David - Father
  • Chris Weitz - Martin Coleman
  • Rachael Huntley - Suzy Coleman
  • Michelle Monaghan- Gwen
  • Benton Jennings - Maitre'D
  • Stephanie March - Julie
  • Jennifer Morrison - Jade
  • Theresa Barrera - Janet
  • Perrey Reeves - Jessie
  • Melanie Tolbert - Jamie
  • Angela Bassett - sauti ya meneja wa Mr. Smith
  • William Fichtner - Dkt Waxleg

[hariri] Mapokezi

Hadi Oktoba 26, 2009, filamu hii imepata mauzo ya $478,336,279 kote duniani..[1]

[hariri] Wimbo

Albamu mbili zilitolewa kutoka kwa filamu hii: moja ikiwa na wimbo uliotungwa na John Powell na nyingine ikiwa na nyimbo zilizotumika kwenye filamu hii. Albamu hizi zilitolewa tarehe tofauti: Juni 28, 2005 na Juni 7, 2005.

[hariri] Marejeo

  1. Mr. And Mrs. Smith. The Numbers. Nash Information Services, LLC. (October 26, 2009). Rudishwa juu ya 2010-01-10.

[hariri] Viungo vya nje

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine