Mponde

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mponde ni kata ya Wilaya ya Bumbuli katika Mkoa wa Tanga, Tanzania.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 10,205 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,232 waishio humo.

Mahali Mponde ilipo[hariri | hariri chanzo]

Kijiji cha Mponde kipo upande wa kusini magharibi mwa mji wa Bumbuli, kijiji cha Mponde kipo kwenye milima na hali ya hewa ya hapa ni baridi. Upande wa magharibi wa kijiji cha Mponde kuna msitu mkubwa sana wa asili ambao ndio unaotenganisha kijiji hiki na kijiji cha Soni.

Historia ya Mponde[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa Mponde ni wasambaa na lugha yao kubwa ni kisambaa na kiswahili.

Kiuchumi[hariri | hariri chanzo]

Shughuli kubwa ya wakazi wa kijiji cha Mponde ni kilimo cha mazao ya chakula na biashara. Katika kijiji cha Mponde kipo kiwanda kikubwa cha kusindika majani ya chai. Hivyo sehemu kubwa ya kijiji hiki imezungukwa na mashamba ya chai.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Bumbuli - Mkoa wa Tanga - Tanzania

Baga | Bumbuli | Dule "B" | Funta | Kisiwani | Kwemkomole | Mahezangulu | Mamba | Mayo | Mbuzii | Mgwashi | Milingano | Mponde | Nkongoi | Soni | Tamota | Usambara | Vuga


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mponde kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.