Morta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Morta

Morta (au morita, pia futuri) ni kipimo cha urefu cha takriban cm 18 - 20.

Ni kati ya vipimo asilia vya Kiswahili, ni umbali mkubwa kati ya kidole gumba na kidole cha shahada kwenye mkono mmoja.

Inafanana na shibiri lakini ni fupi.

Morta si kipimo sanifu, lakini katika maisha ya kila siku inasaidia sana. Mtu akijua urefu wa morta yake anaweza kupima vitu vingi haraka. Kwa sababu mtu hutembea na mkono wake kila saa, tofauti na futi au chenezo. Hivyo kuna ushauri wa kwamba kila mtu apime morta yake na kuikumbuka kwani itamsaidia kila mahali. Kwa kawaida morta ya mtu mzima inaweza kuwa kati sentimita 15-20.