Moneygram

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Moneygram
Ilipoanzishwa1940
Makao MakuuMinneapolis, Minnesota
TovutiMoneyGram
moneyGram

MoneyGram International, Inc ni kampuni ambayo hutoa huduma za kifedha na ina makao yake makuu huko Minneapolis,Minnesota nchini Marekani. Ina vifaa ziada katika sehemu ya Brooklyn Center, Minnesota, Lakewood, Colorado na ofisi za kimataifa katika zaidi ya nchi 170.

MoneyGram International hutoa bidhaa na huduma kupitia mtandao wa mawakala na taasisi za kifedha. Kampuni hii inafanya biashara katika nchi zaidi ya 200 na ina ofisi za mawakala zipatazo 350,000 na mapato ya mwaka ya zaidi dola za Kimarekani bilioni moja.[1]


Kampuni ya Travelers Express Company, Inc, ambayo imekuwa ikiendeshwa tangu mwaka wa 1940, ilinunua MoneyGram Payment Systems, Inc mnamo Juni 1998 kutoka kwa kampuni ya American Express. Biashara ilianzishwa mnamo Desemba 2003 ikihusiana na kujitoa kwake kutoka kwa kampuni mama, Viad Corporation, mwaka wa 2004 na sasa inajulikana kama MoneyGram International.

MoneyGram International hutoa huduma za kutuma fedha. Sehemu nyingine ya MoneyGram International hutoa huduma kwa taasisi za kifedha pamoja na huduma za usindikaji wa malipo.

Habari za hivi karibuni[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 3 Agosti 2009 MoneyGram International, Inc ilisaini mkataba na Affinity Global Services, ya Dallas nchini Marekani, ambayo hutoa teknolojia ya malipo isiyotumlia waya, ili kuwezesha utumaji wa fedha kutumia simu za mkono. "Katika uchumi zinazoendelea, kuna watu wengi wenye simu za mkono kuliko akaunti za jadi za benki. Tunaona nafasi kubwa kuboresha huduma kwa wateja hawa kwa kutoa huduma ya kutuma pesa ili kulipa malipo ya MoneyGram katika fomati mpya kama vile teknolojia ya simu ya mkono, "alisema Anthony Ryan, rais na CEO wa MoneyGram , katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Mshindani mkubwa wa kampuni ya MoneyGram ni Western Union, ambayo ni kubwa na yenye mtandao mpana kuliko MoneyGram.

Onyesho la mchezo wa GSN Bingo Amerika, hutumia mpira mwekundu wenye logo ya MoneyGram; MoneyGram hudhamini mpira huu.


Udanganyifu[hariri | hariri chanzo]

Wahalifu hutumia udanganyifu wa ada ya mapema (419) na mapenzi ya uwongo kuwashawishi waathirika kutuma fedha kupitia huduma ya uhamisho ya "telegraph". Kampuni za Western Union na MoneyGram hudai kuwashauri wateja wao kamwe wasitume pesa kwa watu ambao hawawafahamu.

Mifumo mingine ambayo hutumiwa kwa udanganyifu huhusisha wahusika ambao kuchagua malengo yao kupitia mnada wa mtandaoni kama vile eBay. Wahusika hujitolea kununua bidhaa za bei ghali kutumia huduma za MoneyGram. Kisha tapeli huyu humlipa mhathiriwa wake na kadi karadha iliyoibiwa au malipo mengine kutumia ulaghai, na hii husababisha MoneyGram kuonyesha kuwa biashara hii (transaction) imekamilika. Hii humvutia mhathiriwa katika hali ya usalama wa uongo, na kumsababisha mhathiriwa kutuma bidhaa hizo ambazo anadhani zimelipiwa.

Muda mfupi baadaye, wakati benki ya kutuma inapogundua ulaghai huo wa malipo, "transaction" hiyo hubadilishwa nyuma na mwuzaji hupoteza pesa zilizohamishwa na hakuna njia ya kurudisha bidhaa hizo zilizoibiwa.

MoneyGram imetoa taarifa kwamba wanunuzi ambao hujitolea kulipa kutumia huduma zao kwa wauzaji wasiojulikana hawapaswi kuaminika. Tatizo hili si la MoneyGram pekee, kwani kampuni nyingi za huduma za kifedha zinazofanana hutumiwa kama chombo cha kuendeleza huu udanganyifu.

Njia nyingine ya udanganyifu ni ile ambayo mhalifu anamwuliza mnunuzi kutuma pesa kwa rafiki au jamaa wa mnunuzi kama ushahidi wa imani nzuri. Mhalifu atatuma bidhaa hiyo baadaye na ikipokewa, mnunuzi hugundua uhalifu. Tatizo ni, hata kama mnunuzi atateua sehemu maalum ambapo fedha hii itachukuliwa(yaani karibu na rafiki au jamaa), fedha hiyo inaweza kuchukuliwa na kitambulisho bandia popote duniani. Upande mwingine wa uhalifu huu ni, malipo ya imani nzuri hufanywa kwa rafiki au jamaa kuonyesha ushahidi wa fedha kwa ajili ya nyumba ambayo mnunuzi anajaribu kukodi kutoka kwa mhalifu. Mhalifu atasisitiza kwamba ushahidi uonyeshwe kupitia MoneyGram na si mbinu nyingine yoyote, kama vile fedha ili. Fedha hizi kisha zinapatikana na mhalifu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. MoneyGram. Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-10-24. Iliwekwa mnamo 2017-10-25.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]