Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi
Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi ni uwanja wa shughuli mbalimbali ulioko Kasarani, maeneo ya nje ya Nairobi, Kenya. Uwanja huu una kiwango cha kukimu takribani watu 60,000. Uligharamiwa na Serikali ya Uchina mwaka wa 1987 kwa ajili ya All-Africa Game iliyofanyika mjini Nairobi. Unatumika kwa sasa haswa kwa mechi za kandanda, Timu ya Kitaifa ya Kenya huchezea mechi zake nyingi za nyumbani hapa. Kando na uga wa kandanda, kuna pia ukumbi wa kukimu watu 5,000 wa Gymnasium na ukumbi wa kuogelea kama sehemu ya Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi.
Vilabu za soka kama vile Mathare United na Tusker FC hutumia uwanja huu kwa mechi zao za nyumbani. Kuna uga wa mchezo wa kriketi na uwanja wa gofu zinazojengwa.
Sherehe za mwaka wa 2009 za MTV Africa Music Awards zilifanyikia hapa.
Viungo vya nje [hariri]
- Sports Stadia Management Board - bodi ionayosimamia majumba ya michezo nchini Kenya
- Picha katika worldstadiums.com
- Picha katika fussballtempel.net
Anwani ya kijiografia: 1°13′47.9″S 36°53′32.6″E / 1.229972°S 36.892389°E
| Makala about a Kenyan sports venue bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |