Mohamed Ali Alabbar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alabbar katika foramu ya Kiuchumi ya Dunia ya mwaka 2007

Mohammed bin Amer Al Abbar (pia: Amer Kiarabu: محمد بن علي العبار) ni raia mashuhuri wa Falme za Kiarabu, kutoka Emirate ya Dubai. Yeye ni msaidizi mkuu wa mtawala Dubai na Makamu wa Rais / Waziri Mkuu wa UAE, Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum. Alabbar anatumikia kama Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Uchumi ya Dubai Archived 23 Juni 2004 at the Wayback Machine., na Mwenyekiti wa Emaar moja ya makampuni kubwa zaidi duniani ya kuuza manyumba na ploti. Alabbar pia ni mwanachama wa Baraza la Watendaji ya Dubai.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Kama Mwenyekiti wa Emaar Properties, amechangia pahala pakubwa katika maendeleo ya sekta ya mali isiyohamishika ya Dubai. Emaar, Kampuni ya hisa za pamoja za umma iliyoanzishwa mwaka 1997, imetajwatajwa kwenye Soko la Hisa la Dubai na asilimia kubwa inamilikiwa na Serikali. Emaar Properties kampuni kubwa zaidi miongoni mwa makampuni ya ujenzi na maendeleo katika Uarabuni na imejenga majengo ya makazi na ofisi zaidi ya elfu moja wakati wa ujenzi mwingi sana ulikuwa ukifanyika Dubai. Emaar pia ndiyo iko na wajibu wa kujenga Burj Dubai, ambayo itakuwa muundo mrefu zaidi duniani baada ya kukamilika.

Chini ya Alabbar, Idara ya Maendeleo ya Kiuchumi imeanzisha sera za umma za kuimarisha biashara Dubai na kuanzisha uwazi mkubwa zaidi.

Alabbar pia amechangia katika ukuaji wa sekta zisizo za mafuta Dubai kama Makamu Mwenyekiti wa Dubai Aluminium Company Ltd (DUBAL) 1992-2003. Kutoka 1992-2002 yeye aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Dubai World Trade Centre (DWTC), akiendeleza Dubai kama kitovu cha maonyesho na mikutano.

Alabbar pia ni mwenyekiti wa Emcredit Archived 19 Desemba 2008 at the Wayback Machine., kampuni ya kwanza ya habari ya mikopo ya kujitegemea katika UAE.

Mwaka 2007 Alabbar alienda Korea Kaskazini kuchunguza fursa za uwekezaji huko.[1]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Alabbar alipata shahada yake ya kwanza katika Fedha na Utawala wa Biashara kutoka Shule ya Biashara ya Albers na Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Seattle mwaka 1981. Yeye pia alipata shahada ya udaktari katika humanities kutoka shule aliyokuwa mwaka 2007 [2]

Ushiriki katika vikao[hariri | hariri chanzo]

Alabbar amesema katika vikao kadhaa vya kimataifa, akiwakilisha United Arab Emirates mara kadhaa katika World Economic Forum mjini Davos, Uswisi. Yeye pia huandika mara kadhaa katika foramu za Hammersmad na Westhamfans.

Anachopenda kufanya[hariri | hariri chanzo]

Kama mwanamishezo shadidi, Alabbar alikuwa Mwenyekiti wa [3] Chama cha gofu cha UAE (sasa Shirikisho la Gofu la Emirates)], ambayo inakuza mashindano ya kila mwaka ya gofu ya PGA Dubai Desert Classic. Nafasi yake ilichukuliwa na HE Sheikh Fahim Al Qassimi. Alabbar alitajwa hivi karibuni kama wachezaji gofu wenye haiba kumi bora duniani na [4] Golf World magazine . Atakuwa mwenyeji wa toleo la Kiarabu la progralu la televisheni la The Apprentice iitwayo el idara jadara .

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [0] ^ Tajiri wa Dubai atembelea Pyongyang Forbes, 9 Septemba 2006
  2. "Emaar Chairman receives honorary doctorate from Seattle University", Eye of Dubai, 20 Juni 2007. Retrieved on 18 Juni 2009. Archived from the original on 2011-10-04. 
  3. Shirika la Gofu la UAE. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-07-26. Iliwekwa mnamo 2010-01-05.
  4. [4] ^ Dunia ya Gofu

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]