Mnandi-pwani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mnandi
Mnandi-pwani mkubwa (Fregata minor)
Mnandi-pwani mkubwa (Fregata minor)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Suliformes (Ndege kama ndegejinga)
Familia: Fregatidae (Ndege walio na mnasaba na minandi-pwani)
Jenasi: Fregata
Lacépède, 1799
Ngazi za chini

Spishi 5:

Minandi-pwani ni ndege wa bahari wa jenasi Fregata, jenasi pekee ya familia Fregatidae. Wana domo refu lenye ncha kwa kulabu, mabawa marefu na mkia wenye panda. Rangi yao ni nyeusi; jike ana tumbo jeupe na dume ana mfuko wa koo mwekundu ambao anaweza kumvimbisha ili kumvutia jike. Ndege hawa hawaogelei na watembea kwa shida, kwa hivyo wako hewani takriban saa zote. Wanaweza kukaa hewani hata zaidi ya wiki moja. Kama shakwe-waporaji, huonekana mara nyingi wakipora mateka kwa ndege wengine, lakini chakula chao hasa ni samaki, ambao huwakamata wakiruka, na kwa kiasi kidogo zaidi makinda ya ndege. Jike hutaga yai moja au mayai mawili juu ya mti au ardhini au juu ya mwamba wa pwani.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi ya bara jingine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]