Mlima Longonot

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mlima Longonot, Kenya.

Mlima Longonot ni volkeno ya kale yenye kimo cha mita 2776 juu ya UB iliyoko kusini mwa Ziwa Naivasha katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, kaunti ya Nakuru, nchini Kenya, Afrika. Inadhaniwa kulipuka kwa mara ya mwisho katika miaka ya 1860.

Jina lake linatokana na neno la Kimasai oloonong'ot, maana yake "milima yenye pembe nyingi" au "miinuko matuta".

Mlima Longonot unalindwa na Shirika la Wanyamapori la Kenya kama sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Longonot.

Kilele cha Mlima Longonot una kasoko yenye kipenyo cha kilomita 1.8 na urefu wa mita 200 au zaidi kwenda chini kutegemeana na urefu wa kuta za kasoko. Njia nyembamba inaelekea kutoka kiingilio cha mbuga hadi mdomo wa volkeno, na kuendelea kwenye kona ya kasoko ya volkeno. Ziara nzima ni kilomita 8-9 tu lakini ina mwinuko sana, hivi kwamba safari ya kutoka lango la Hifadhi hadi kilele cha Longonot na kurudi tena langoni huchukua takriban masaa 5 kwa miguu. Lango liko aghalabu mita 2150 juu ya usawa wa bahari na upeo unafikia mita 2760 m juu ya usawa wa bahari lakini kufuatia mzunguko wake usio sawa kunahusisha zaidi ya tofauti ya mita 630.

Msitu wa miti midogo unapatikana kwenye sakafu ya volkeno, na matundu madogo ya mvuke yanapatikana yamewekwa kuzunguka kuta za volkeno. Mlima huu ni makao kwa aina mbalimbali ya wanyamapori, hasa pundamilia na twiga na nyati (mbolea kwenye mdomo) na hartebeest. Chui pia wameripotiwa kuonekana lakini ni vigumu sana kuwapata.

Mlima Longonot uko kilomita 60 kaskazini magharibi mwa Nairobi na inaweza kufikiwa kutoka huko kwa barabara ya lami. Barabara hiyo ilifanyiwa ukarabati na EU na sasa ni bora, na imepunguza muda wa kusafiri kutoka Nairobi kuwa saa moja. Mji wa karibu pia unaitwa Longonot. Stesheni ya setlaiti ya Longonot iko kusini mwa mlima huu.

Tarehe 21 Machi 2009 mioto ya vichaka ilichoma pande za mlima na kuzamia katika volkeno, ikawanasa wanyamapori waliokuwa wakila majani yaliyokumbwa na ukame.[1]

Kituo cha Ardhini cha Longonot 2010

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]