Mkutano wa Berlin wa 1885

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mkutano wa Berlin wa 1885

Mkutano wa Berlin wa 1885 (Kijerumani: "Kongokonferenz" yaani "mkutano juu ya Kongo") ilikuwa mkutano wa kimataifa kuhusu athira ya nchi za Ulaya katika Afrika uliofanyika kati ya 15 Novemba 1884 hadi 26 Februari 1885 Berlin mji mkuu wa Ujerumani. Matokeo yake yalikuwa "Azimio la Berlin" (Kongoakte; General Act of the Berlin Conference) lililoweka msingi kwa ugawaji wa Afrika kati ya madola ya Ulaya.

Utangulizi[hariri | hariri chanzo]

Kufifia kwa ukoloni mwanzo wa karne ya 19[hariri | hariri chanzo]

Kwa sehemu kubwa ya karne ya 19 mataifa ya Ulaya hayakutafuta utawala katika Afrika. Vituo mbalimbali vilivyoanzishwa katika karne za 17 na 18 kwenye pwani za Afrika zilikwama tena kwa sababu gharama na faida hazikulingana. Hasa kupigwa marufuku kwa utumwa kulipunguza faida za koloni hizi zilizokuwa dogo na zaidi vituo vya kibiashara na vya kijeshi kwa ajili ya mawasilano baharini.

Mataifa ya Ulaya hayakujaribu sana kupanusha utawala wao barani. Sifa za koloni zilipungua kwa jumla kwa sababu nchi mbalimbali zilipoteza koloni zao baada ya kuasi kwa walowezi huko Amerika ya Kaskazini dhidi ya Uingereza (Marekani), huko Amerika ya Kusini dhidi ya Hispania (mataifa mapya ya Amerika Kusini) na uasi wa watumwa wa Haiti dhidi ya Ufaransa. Watu wengi waliuliza maswali juu ya faida ya kuwa na koloni kama wachache walitajirika lakini umma ilipaswa kugharamia bei za vita na jeshi.

Kuangalia Afrika upya[hariri | hariri chanzo]

Lakini katika sehemu ya pili ya karne Afrika ilianza kuvuta wafanyabiashara wa Ulaya upya kwa sababu mapinduzi ya viwandani yalihitaji mafuta yaliyopatikana kutokana na mawese ya kutia grisi mashine za viwandani. Mafuta haya yalipatikana katika nchi za Guinea hasa eneo la delta ya mto Niger. Serikali za Ulaya zilijaribu kuhakikisha kipaumbele na faida kwa wanafanyabiashara kutoka kwao. Hali hii ilianzisha mashindano kati ya nchi hizo.

Kuanzia mwaka 1869 mfereji wa Suez ilifunguliwa. Uingereza, Ufaransa na Italia zilishindana kukamata vituo vya kijeshi kando la mlangobahari wa Bab el Mandeb kwa nia ya kuhakikisha athira yao juu ya njia hii ya mawasiliano.

Safari za Henry Morton Stanley katika beseni ya mto Kongo ziliondoa madoa meupe kwenye ramani za Afrika. Mfalme Leopold II wa Ubelgiji alimwajiri Stanley aliyejenga misingi ya utawala wa Leopold huko Kongo.

Mashindano juu ya utawala wa Afrika[hariri | hariri chanzo]

Katika miaka tangu 1880 nchi mbalimbali za Ulaya zilianza kuvamia sehemu za bara la Afrika kwa sababu tofautitofauti. Sababu muhimu ilikuwa maendeleo makubwa ya teknolojia katika nchi za viwandani yaliyosababisha uwezo wao wa kijeshi kupita uwezo wote wa jamii zisizoingia bado katika ngazi hii ya kiuchumu. Kwa lugha nyingine: gharama za kuvamia nchi isiyo ya viwandani zilipungua haraka. Mwendo huu ulisababisha mashindano kati ya nchi zilizoendelea na hofu ya nchi nyingine kupata kipaumbele.

  • 1881: Ufaransa ilivamia Tunisia (kwa kusudi la kuhakikisha malipo ya madeni ya serikali ya Tunisia);
  • 1881: Ufaransa ilianza pia kutawala Kongo ya Kifaransa kwa njia ya mikataba ya ulinzi kwa kusudi la kupakana uenezaji wa utawala wa Leopold II.
  • 1882: Uingereza ulivamia Misri kwa kusudi la kutawala mfereji wa Suez. Misri iliendela kama nchi huru kwa jina lakini hali halisi ilikuwa nchi lindwa. Kwa njia hii Uingereza uliingizwa katika siasa za Sudan na Somalia ambako Misri iliwahi kuwa na maeneo na vituo.
  • 1882: Italia kuvamia sehemu za Eritrea.

Chanzo[hariri | hariri chanzo]

Chanzo cha mkutano ulikuwa fitina kati ya Ureno na Dola huru la Kongo la mfalme Leopold II wa Ubelgiji juu ya utawala wa mdomo wa mto Kongo. Ureno ilikumbuka mkataba wake wa karne mingi na ufalme wa Kongo na kudai pwani lote pamoja na mdomo wa mto mkubwa ni yake. Leopold alitegemea njia ya mto kwa mawasiliano yake alihitaji kanda la eneo hadi baharini. Uingereza ulisimama upande wa Ureno. Bismarck alikuwa tayari kupatanisha nchi hizi na kuongeza msimamo wake wa kidiplomasia.

Habari za mkutano ziliharakisha jitihada za kusimamisha bendera za Ulaya kwenye ardhi ya Afrika. Mwaka 1984 uliona wimbi la matangazo ya maeneo ya Afrika kuwa eneo lindwa la Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Italia. Mara nyingi sababu ya kutangaza madai au eneo lindwa ilikuwa hofu ya nchi nyingine kusimamisha bendera yake palepale. Wapelelezi na wanfanyabiashara walijitahidi kuweka msingi wa koloni kabla ya mkutano wa Berlin kwa tumaini ya kwamba maazimio yake yatathebitisha madai yao.

Kati ya wapelelezi waliokazia jitihada alikuwa Mjerumani Karl Peters aliyezunguka katika Afrika ya Mashariki dhidi ya ushauri wa serikali yake akikusanya sahihi za machifu waliotia dshihi miktaba naye bila kuelewa walichofanya. Kabla ya mkutano na wakati wa mkutano mwenyewe Peters aliweka msingi wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ya baadaye.

Washiriki[hariri | hariri chanzo]

Nchi zifuatazo zilishiriki mkutanoni chini ya uwenyekiti wa Chansella Bismark:


Maazimio[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]