Mivigha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mivigha ni sherehe zinazofanywa na makabila mbalimbali kwa lengo au tukio maalumu la kabila husika.

Sherehe hizo mara nyingi huambatana na matukio mbalimbali kulingana na jamii husika, kwa mfano kucheza ngoma ya kabila husika.

Mfano wa mivigha ni sherehe za jando na unyago zinazofanywa na jamii mbalimbali kwa namna tofautitofauti kwa madhumuni au kusudi la kuwafundisha na kuwaasa vijana katika maisha yao ya kila siku.

Mara nyingi katika jamii za Kiafrika, hasa Tanzania, neno "jando" linahusisha malezi kwa vijana (wanaume) na "unyago" linahusisha malezi kwa vijana (wanawake) ingawa yapo baadhi ya makabila, ambapo maneno hayo yanahusishwa kama ni mafunzo kwa wote, bila kujali vijana wa kiume au wa kike.

Jando na unyago huhusisha kuingia kwa mwanajamii kwenye kundi la watu wa aina fulani kutoka kundi la aina nyingine. Mfano harusi, kutawazwa chifu n.k.

Katika sherehe hizi pia mtu hutolewa kutoka kundi la watoto na kuingia kundi la watu wazima.

Katika mivigha kuna wahusika wa aina kuu tatu: (i) Mtendaji/Watendaji - Ni wale wote wanaoshiriki kutenda ile dhana ya kuwatoa watu kutoka kundi moja kwenda kundi lingine. (ii) Watendwa - Ni wale wanaoingia kutoka kundi moja kwenda lingine. Hawa ndio ambao vitendo vinafanyika juu yao ili waone na wajifunze na ikiwezekana wavifanyie utekelezaji. (iii) Waangaliaji - Ni wale wanaoangalia mambo yanayotendeka bila wao kushiriki katika kucheza au kuimba au kutoa mafunzo. Wao wanaangalia tu.

Jamii nyingi za Kiafrika, hasa Tanzania, inaamini kwamba mivigha ina umuhimu mkubwa katika jamii zao. Umuhimu ni:

  1. Kufundisha kazi, kama vile: kilimo, ufugaji n.k
  2. Kuhimiza umuhimu wa ujasiri katika maisha
  3. Kufundisha suala zima la unyumba na malezi
  4. Hufundisha umuhimu wa umoja na mshikamano katika maisha.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mivigha kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.