Mita ya ujazo
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mita moja ya ujazo ya saruji
Mita ya ujazo (kifupi m³) ni kipimo cha mjao chenye urefu, upana na kimo cha mita moja. Ni kiwango katika vipimo vya SI. Jina lingine ni "kilolita".
Mita moja ya ujazo inalingana na lita 1,000 au sentimita za ujazo 1,000,000.
1 m³ ya maji safi katika hali sanifu (halijoto ya 3.98 °C) na shindikizo sanifu ya hewaanga) huwa na masi ya kilogramu 1,000.
Kifupi kingine ni CBM kwa Kiing. "cubic meter" hasa katika hati za biashara na usafirishaji.