Misigiri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Misigiri ni mji mdogo katika kata ya Ulemo kwenye Wilaya ya Iramba (Mkoa wa Singida, Tanzania). Msigiri inapitiwa na barabara kuu kutoka Dodoma iendayo Mwanza mpaka nje ya nchi kama Kongo, Rwanda na Burundi.

Idadi ya wakazi imeongezeka kutokana na usafiri ulioboreshwa na nafasi za kiuchumi kama vile biashara, kilimo na uchimbaji wa madini ya dhahabu. Kuna kilimo cha mazao ya biashara kama vile alizeti na karanga.