Mipango miji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mpango miji wa mji mkuu wa Minnesota
Mpango mji

Mipango miji ni sayansi na sera kuhusu maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kimazingira katika miji na vitongoji vyake. Mgiriki Hippodamus anasemekana kuwa ndiye baba wa mipango miji kutokana na ubunifu wake wa mji wa Miletus ingawa kumekuwa na miji iliyopangwa kabla yake.

Taaluma ya mipango miji imechipuka toka kwenye taaluma za usanifu majengo na uhandisi.