Miombo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Msitu wa miombo katika kaskazini ya tambarare ya Nyika, Malawi

Miombo ni aina ya miti inayoitwa na wanabiolojia kwa jina brachystegia. Miti hii inaunda misitu isiyo minene hasa katika mazingira makavu kiasi ya Afrika ya Mashariki na Kusini hasa katika nchi Zimbabwe, Zambia, Msumbiji, Angola, Tanzania na Malawi. Misitu ya miombo inafunika maeneo ya kilomita za mraba milioni 5.

Misitu ya miombo humwaga majani wakati wa majira ya ukame kwa kusudi la kuhifadhi maji ndani yao. Kabla ya kuja kwa majira ya mvua huotesha majani mapya. Wakati wa mabadiliko haya majani yanaonyesha rangi za dhahabu na nyekundu zinazopendeza.

Miombo inayopatikana mara yingi ni hasa Brachystegia boehmii und B. longifolia.[1]

[hariri] Miombo na watu

Misitu ya miombo ni muhimu kwa maisha ya watu wanaoishi karibu nayo wakivuna hapa matunda, asali, kuni na lishe kwa mifugo. Kukatwa kwa miti hii imezidi kutokana na kuongezeka kwa watu na matumizi ya kuni. Utengenezaji wa makaa karibu na barabara kubwa yanayopelekwa mjini ni sababu muhimu. Katika maeneo ambako tumbako hulimwa wakulima wanakata miti mingi mno wakitumia kuni kukausha majani ya tumbako.

[hariri] Wanyama

Miombo inaota kwenye ardhi isiyo na rutba sana. Hata hivyo misitu ya miombo ni nyumbani kwa spishi nyingi za wanyama pamoja na ndege wanaoishi hapa pekee. Wanyamapori wengi wanapata kinga na lishe kati ya miti hii kama vile tembo, mbwa mwitu, na wengine.


[hariri] Marejeo na Viungo vya Nje

  1. Smith, Paul & Allen, Quentin: Field Guide to the Trees and Shrubs of the Miombo Woodlands, Royal Botanic Gardens, Kew 2004.
Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine