Milenia ya 6 KK

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Lango la Historia | Lango la Biografia | Karibuni | Orodha ya Miaka

| Milenia ya 7 KK | Milenia ya 6 KK | Milenia ya 5 KK |

Makala hii inahusu milenia ya 6 KK (miaka 5999 KK - 5000 KK). Katika sehemu nyingi zha dunia tunaona vyanzo vya kilimo.

Matukio[hariri | hariri chanzo]

 • Kisiwa cha Britania (Uingereza) hutenganishwa kutoka kwa Ulaya bara kwa kupanda ya uwiano wa bahari. Sababu yake ni badiliko la halijoto linalosababisha kuyeyuka kwa barafuto nchani na barafu hii kuwa maji mengi yanayopandisha uwiano wa bahari.
 • Mnamo 5800 KK kunatokea banguko kubwa chini ya bahari kwenye tako la bara karibu na pwani la Norwei (banguko la Storegga). Banguko ilisababisha tsunami iliyoharibu vijiji vya watu huko Uskoti.
 • katika eneo la Mediteranea hali ya hewa ni ya kitropiki
 • Misri kuna kilimo kwenye bonde la Naili
 • plau inagunduliwa
 • tangu 6000 KK: kuku wanaanza kufugwa nchini China
 • tangu 6000 KK: mizabibu ya kwanza inapandwa katika Kaukazi na Mesopotamia.
 • tangu 5600 KK: kilimo kinaanza Ulaya ya Kati
 • tangu 5600 KK: Eneo la Sahara linazidi kuwa kabisi na kuwa jangwa; watu huondoka.
 • mnamo 5500 KK: umwagiliaji wa mashamba katika Mesopotamia
 • mnamo 5500 KK: vifaa vilivyofinyangwa vya kwanza katika Asia kusini
 • baina 5500 na 5300 KK: mtama unaanza kulimwa huki China Kaskazini
 • mnamo 5200 KK: hekalu za kwanza katika Mesopotamia
 • mnamo 5100 KK: Mahindi, maharagwe, mboga na maparachichi hupandwa katika Amerika ya Kati
 • mnamo 5000 KK: Mpunga hulimwa kwenye pwani la China


Watu[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Einzelnachweise[hariri | hariri chanzo]