Mikrowevu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Masafa ya mawimbi (wavelength) ya mikrowevu iko kati ya mawimbi ya redio na infraredi katika spektra ya mawimbi ya sumaukumeme

Mikrowevu (pia: wimbi mikro; kutoka Kiingereza microwave) ni aina ya mawimbi ya sumakuumeme inayofanana na mawimbi ya redio, lakini masafa ya mawimbi (wavelength) yake ni mafupi zaidi. Haionekani kwa macho ya binadamu. Masafa ya mikrowevu yako kati ya mita 1 hadi milimita 1; marudio (frequency) ni kati ya 300 MHz (0.3 GHz) na 300 GHz.

Matumizi ya mikrowevu

Katika maisha ya kila siku mikrowevu zinajulikana zaidi kutokana na matumizi yake katika majiko ya kupashia moto chakula.

Lakini zinatumiwa katika teknolojia ya mitambo mingi pamoja na rada, mawasiliano ya simu za upepo, bluetooth na waifai. Kuna uchunguzi kwa matumizi yake ya kijeshi, yaani kama silaha.

Mikrowevu kama jiko

Jiko la mikrowevu linafanya kazi kwa sababu mawingu yake yanaathri molekuli ya maji ndani yake kujipanga kama sumaku ndogo. Baadaye mwelekeo unabadilishwa kinyume. Kwa njia hiyo molekuli za maji ndani ya jiko zinachezacheza. Mwendo huu unaongeza kiwango cha joto ya maji na kwa njia hiyo ya kila kitu chenye unyevu ndani yake kilichopo ndani ya jiko la mikrowevu.

Kwa njia hiyo vyakula vyenye maji ndani yake vinaweza kupashwa moto haraka sana. Ila tu matoleo si mazuri kwa vyakula vikavu sana.

Vilevile vitu vilivyojengwa kwa molekuli zisizokubali kuathiriwa kisumaku hazipashwi moto. Kumbe aina za plastiki zinaweza kukaa kwenye mikrowevu bila matata yaani chakula kinakuwa cha moto lakini sahani ya plastiki ya kufaa inabaki baridi.

Viungo vya Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mikrowevu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.