Meru (Kenya)
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Meru ni sehemu ya kati ya Mkoa wa Mashariki nchini Kenya upende wa mashariki-kaskazini ya mlima Kenya. Inakaliwa na Wameru.
Eneo la Meru lilijumlishwa hadi 1992 katika wilaya ya Meru iliyogawiwa baadaye kuwa wilaya zifuatazo:
- Meru Kati (majimbo ya uchaguzi wa South Imenti, Central Imenti, North Imenti)
- Meru Kaskazini iliyogawiwa tena kuwa wilaya za
- Tigania
- Nyambene (majimbo ya uchaguzi Tigania East, Igembe, Tigania West na Ntonyiri)
- Meru Kusini (jimbo la uchaguzi laitwa Nithi)
- Tharaka
Sehemu kubwa ya Meru ina ardhi ya rutba na mvua ya kutosha