Mirerani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mererani)

Mirerani ni kata ya Wilaya ya Simanjiro katika Mkoa wa Manyara, Tanzania.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,450 waishio humo. [1] lakini hali halisi idadi ya wakazi ni kubwa zaidi kutokana na uchimbaji na biashara ya vito vya tanzanaiti.[2]

Katika milima iliyopo karibu na mji huu kuna migodi mingi ambako vito vya tanzanaiti kuchimbwa. Hata kama hapa ni mahali pekee duniani ambako vito vilivyopendwa vya tanzanaiti vinapatikana bado Mererani ni mahali pa umaskini ila dalili nyingi za maendeleo.[3]

Uchimbaji wa madini[hariri | hariri chanzo]

Eneo ambako tanzanaiti inapatikana line urefu wa kilomita 50 na upana wa kilomita mbili.[4] Tangu kugunduliwa kwa tanzanaiti mnamo mwaka 1967 kampuni ya kiserikali ya Tanzania Gemstone Industries (TGI) ilipewa haki ya pekee ya kuchimba vito Mererani. TGI ilishindwa kuendesha kazi hii; ikaruhusu wachimbaji wadogo kuanzisha migodi pia kwa masharti ya kwamba wangehitaji kuuza vito vyote kwa kampuni. Lakini mapato yalikuwa duni mno, inaaminiwa kuwa sehemu kubwa ya vito haikuonyeshwa na kupelekwa nje ya nchi kwa siri. TGI ikatoka mnamo 1986 wakati serikali iliruhusu makampuni ya kigeni kufanya shughuli nchini. Wachimbaji wadogo wa binafsi waliingia katika sehemu zilizowahi kumilikiwa na TGI.

Mwaka 1991 serikali iligawa eneo limegawiwa katika kanda nne zinazoitwa Block A, B, C na D. Wachimbaji wadogo walipewa block D, wafanyabiashara Watanzania walipewa block A na B. Block C ilipewa kwa kampuni ya Graphtan, ushirikiano wa TGI na kampuni ya Kiingereza. Graphtan walilenga si vito bali minerali ya grafati (ing. graphite). Baada ya kushindwa kwa Graphtan haki za kuchimba kwenye Block C ilinunuliwa kwanza na kampuni ya Afrika Kusini Mererani Mining Ltd iliyonunuliwa mwaka 2004 kampuni ya TanzaniteOne ambayo ni kampuni ya kigeni ulioandikishwa kwenye visiwa vya Bahama.

Leo hii TanzaniteOne inaendelea kuchimba vito katika mashimo ya migodi sita yenye kina cha mita 250 hadi 350. Kampuni inaajiri wafanyakazi 560. Block B na D zinachimbwa na wachimbaji wadogo na kuna mashimo yapatao 700 [5]. Makampuni ya Kilimanjaro Mining na Tanzanite Africa Ltd. yanachimba kwenye Block A na pia kando la Block D yote mawili ni makampuni ya Kitanzania.

Vito vya tanzanaiti vinapatikana chini ya ardhi katika mabonge hapa na pale; wachimbaji wanaweza kuendelea kwa siku au hata miezi bila kukuta kitu. Migodi ya pekee inayoendelea kutoa vito mfululizo ni ya TanzaniteOne.

Mara kwa mara kuna matizo kati ya kampuni kubwa na wachimbaji wadogo ilhali kampuni inalalamika ya kwamba wachimbaji wadogo wanaingia ndani ya block C kutoka chini ya ardhi na kuvuna kwa siri[6]. Vivyo hivyo wachimbaji wazalendo mara nyingi wanasikitika kuwepo kwa kampuni ya kigeni.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Simanjiro - Mkoa wa Manyara - Tanzania

Emboreet | Endiamutu | Endonyongijape | Kitwai | Komolo | Langai | Loiborsoit | Loiborsiret | Mirerani | Msitu wa Tembo | Naberera | Naisinyai | Ngorika | Oljoro No.5 | Orkesumet | Ruvu Remit | Shambarai | Terrat


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Manyara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mirerani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.