Melanesia
Melanesia ni eneo la Bahari ya Pasifiki kaskazini ya Australia. Ni moja kati ya makundi makubwa matatu ya visiwa vya Pasifiki pamoja na Mikronesia na Polynesia.
Jina lake limeundwa na maneno ya Kigiriki ya νῆσος kisiwa na μέλας cheusi yaani "visiwa vyeusi". Mpelelezi na nahodha Mfaransa Jules Dumont d'Urville alitunga jina hili 1832 akitaka kutaja tabia ya wakazi wazalendo waliokuwa na rangi nyeusi-nyeusi.
Watu na utamaduni [hariri]
D'Urville alijumlisha wakazi wa visiwa hivi pamoja kutokana na rangi yao. Lakini hali halisi ni watu wa aina mbalimbali. Wengine ni Waaustronesia, wengine Wapapua na wengine watu kutokana na mchanganyiko wa vikundi hivi viwili.
Nchi za Melanesia [hariri]
Fiji, Papua Guinea Mpya, Visiwa vya Solomon, Vanuatu na Kaledonia Mpya (chini ya Ufaransa) zinajihesabu kuwa sehemu za Melanesia. Kuhusu visiwa vingine mawazo hutofautiana.
Visiwa vya Melanesia [hariri]
Visiwa na funguvisiwa zifuatazo zinahesabiwa katika Melanesia:
- Funguvisiwa ya Bismarck
- Fiji
- Kaledonia Mpya
- Guinea Mpya (Papua Guinea Mpya pamoja na jimbo la Papua la Indonesia).
- Visiwa vya Maluku
- Visiwa vya Solomon
- Visiwa vya Torres Strait
- Vanuatu
- Palau
Visiwa vilivyoko katika eneo hili lakini wakazi hawajitazami kuwa Wamelanesia:
Wakati mwingine hata visiwa upande wa Guinea Mpya vinahesabiwa humo ingawa wakazi hawajitazami hivyo: Halmahera, Alor na Pantar.
| Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Melanesia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |