Mdumu mwitu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Midumu mwitu wa Marekani ya kaskazini ni wa jinasi ya Sarracenia na wao huwa na matawi yanayosimama wima.

Mdumu mwitu ni mmea unaokula nyama kwa kutumia mtego uliochimbuka wenye maji ndani. Imedhaniwa kuwa mitego hii yenye maji ndani iliibuka kutoka matawi yaliyojikunja, huku mabadiliko ya viumbe yakipendelea matawi yenye michimbuko mikubwa zaidi katika kipindi cha miaka mingi.

Hata hivyo, baadhi ya midumu mwitu wa jenasi kama ile ya Nepenthes wanajumuishwa katika kikundi tofauti cha mimea wenye matawi kama karatasi yenye gundi. Hili linaonyesha kuwa mtazamo kuwa midumu mwitu iliibuka kutoka matawi yaliyojikunja huenda hukawa si wa kweli.

Bila kujali jinsi mmea huu ulivyobadilika, wadudu wanaotambaa na wanaoruka ikiwemo nzi huvutiwa kwa mchimbuko huo ulioundwa na tawi, mara nyingi kwa rangi na maji yenye sukari. Pande za tawi huenda zikawa zinateleza na zimeumbwa kwa njia inayowafanya wadudu washindwe kutoka pindi wanapoingia ndani.

[hariri] Marejeleo zaidi

  • Schnell, Donald (2003). Carnivorous Plants of the United States and Canada. Second Edition. Timber Press, Oregon, U.S.A.
Greentree.jpg Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdumu mwitu kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine