Mdiria
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Mdiria | ||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Midiria ni ndege wadogo wa nusufamilia Alcedininae katika familia Alcedinidae. Spishi nyingine zinaitwa kizamiadagaa au kisharifu. Spishi zote zina rangi buluu mgongoni na kichwani, na tumbo ni jekundu kwa kawaida. Ndege hawa wana domo kubwa kwa kulinganisha na ukubwa wao ambalo lina ncha kali. Hukamata samaki wakipiga mbizi majini lakini hula gegereka na wadudu pia. Visharifu hula wadudu tu. Dume na jike pamoja huchimba tundu katika ukingo wa mto au uso mwingine wa wima wa mchanga. Tundu hili lina urefu wa mita 0.5-1 na jike huyataga mayai 2-10 kwenye mwisho wake uliokuzwa.
[hariri] Spishi za Afrika
- Alcedo atthis Mdiria wa Ulaya (Common Kingfisher)
- Alcedo cristata Kizamiadagaa (Malachite Kingfisher)
- Alcedo leucogaster Mdiria Tumbo-jeupe (White-bellied Kingfisher)
- Alcedo nais Mdiria wa Principe (Príncipe Kingfisher)
- Alcedo quadribrachys Mdiria Buluu (Shining Blue Kingfisher)
- Alcedo semitorquata Mdiria Ukosi-buluu (Half-collared Kingfisher)
- Alcedo thomensis Mdiria wa Sao Tome (São Tomé Kingfisher)
- Alcedo vintsioides Mdiria wa Madagaska (Madagascar Kingfisher)
- Ceyx (au Ispidina) lecontei Kisharifu Mdogo (Dwarf Kingfisher)
- Ceyx (au Ispidina) madagascariensis Kisharifu wa Madagaska (Madagascar Pygmy Kingfisher)
- Ceyx (au Ispidina) picta Kisharifu (African Pygmy Kingfisher)
[hariri] Spishi za mabara mengine
- Alcedo argentata (Silvery Kingfisher)
- Alcedo azurea (Azure Kingfisher)
- Alcedo coerulescens (Cerulean Kingfisher)
- Alcedo cyanopectus (Indigo-banded Kingfisher)
- Alcedo euryzona (Blue-banded Kingfisher)
- Alcedo hercules (Blyth's Kingfisher)
- Alcedo meninting (Blue-eared Kingfisher)
- Alcedo pusilla (Little Kingfisher)
- Alcedo websteri (Bismarck Kingfisher)
- Ceyx erithacus (Black-backed Kingfisher)
- Ceyx fallax (Sulawesi Kingfisher)
- Ceyx lepidus (Variable Kingfisher)
- Ceyx melanurus (Philippine Dwarf Kingfisher)
- Ceyx rufidorsa (Rufous-backed Kingfisher)