Matumizi ya Lugha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Matumizi ya lugha hutahini uwezo wa mwanafunzi wa kuelewa na kukitumia Kiswahili kwa kuongea na kuandika.

Vipashio vya lugha

Lugha huundwa na:

Sauti za Kiswahili

Huwa mbili:

-->Irabu ni tano. (a, e, i, o, u)

Irabu na Konsonanti (Matamshi na aina) Unapotamka irabu, hakuna hewa inayozuiliwa lakini konsonanti zinapotamkwa, hewa huzuiliwa na ala za matamshi.
Kutamka Irabu(ulimi na midomo hutumika)
--e, i: Ni za mbele ya ulimi, midomo imetandazwa.
--a  : Ni ya kati ya ulimi, midomo imetandazwa, ulimi huinuka na kutandazwa.
--o, u: Ni za nyuma ya ulimi, midomo imeviringwa.

>>Aina za Konsonanti

Silabi mwambatano

Mifano ya silabi mwambatano: --bw: bwaga, bweka --nd: ndimu, ndoa, ndugu

Kuchanganua Sentensi (sawa na kupambanua/kuainisha)

Kuna njia tatu:

Matumizi ya PO

  • i. Kuonyesha wakati

Mfano: Alipoenda alikuwa amechelewa.

  • ii. Kuonyesha mahali

Mfano: Hapo pananuka.

Matumizi ya KWA

  • a. Kuonyesha mahali

Hadija yuko kwa Mwangi.

  • b. Kuonyesha chombo cha utendaji

Alisafiri kwa basi

  • c. Jinsi

Alimfokea kwa ghamidha

  • d. Umilikaji wa mahali

Hujafika kwao.

  • e. Kuonyesha uhusiano wa sehemu ya kitu kizima

Mbili kwa tano (2/5)

Ni kwa nini umetenda haya?

  • g. Kuonyesha muda ambapo jambo lilitendeka

Alifungwa jela kwa miaka kumi.

  • h. Sababu/nia

Aliadhibiwa kwa utundu wake.

  • i. Kuonyesha mfululizo wa utendaji wa jambo

i.Ujumbe ule ulipelekwa moja kwa moja ii.Walikaa sako kwa bako.

  • j. Kuonyesha matokeo ya jambo

Alisoma kwa hivyo akapita mtihani

  • k. Kuonyesha muda

Alikaa huko kwa muda wa siku nyingi.

  • l. Kama kilinganishi

Walipata magoli matano kwa nunge.

i.Kuonana uso kwa uso ii.Beba kwa bega